Na
Chalila Kibuda, Globu ya jamii
FAMILIA
ya Ruge Mutahaba imetoa utaratibu wa mazishi ya ndugu yao, ambayo yanatarajiwa
kufanyika wiki ijayo mkoani Kagera.
Akizungumza
leo jijini Dar es Salaam ,Msemaji wa familia ya Ruge, aliyejitambulisha kwa
jina la Kashasha amesema mipango
iliyopangwa na familia ni kuhakikisha wanaufikisha mwili wa Ruge Dar es Salaam
siku ya Ijumaa na kuagwa Jumamosi katika ukumbi wa Karimjee.
"Familia
imeamua kwamba mwili wa ndugu yetu Ruge utapumzishwa nyumbani mkoani Bukoba
siku ya Jumatatu.Siku hiyo ndio tutampumzisha katika nyumba yake ya
milele,"amesema.
Ruge
Mutahaba aliyezaliwa mwaka 1970, ni mmoja wa waasisi na Mkurugenzi wa
Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group amefariki dunia jana jioni Februari
26 akiwa Afrika Kusini ambako alikuwa anapatiwa matibabu.
ikumbukwe
kuwa Ruge ni mmoja wa waanzilishi na waasisi wa Clouds Media.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...