Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeendelea na Kampeni yake katika Wilaya ya Tarime na Rorya ya kutoa Elimu kwa umma juu ya umuhimu wa kununua bidhaa zilizothibitishwa ubora wake na TBS na jinsi gani wajasiriamali wanaweza kupata Leseni ya TBS bure bila gharama yoyote.

Kampeni hiyo ya Elimu kwa umma imefanyika Maeneo ya Soko jipya la REBU,Stendi ya Tarime Mjini,Mnada wa Mtana na maeneo mengine ya Halmashauri ya Mji na Wilaya.

wananchi walijitokeza kupata elimu sambamba na ufahamu wa masuala mbalimbali yahusuyo Ubora wa Bidhaa.Kwa upande wake Afisa Udhibiti ubora, Mhandisi Paul Ndege amezidi kuwakumbusha Wananchi wote kuwa vita ya bidhaa hafifu sio ya TBS pekee bali ya kwetu sote, Hivyo,wasisite kutoa taarifa kupitia mawasiliano waliyopewa pale wanapogundua uwepo wa bidhaa hafifu katika soko lao na kuhakikisha wananunua bidhaa zilizothibitishwa na TBS.

Vilevile Shirika lilipata fursa ya kutoa semina kwa wajasiriamali wanaojihusisha na bidhaa mbalimbali kama nafaka,sabuni, maziwa,asali na unga lishe,juu ya utaratibu wa kupata leseni ya kutumia alama ya ubora ya TBS na kuwa huduma hiyo inatolewa bure kwa wajasiriamali wadogo.

Wajasiriamali wengi walionyeshwa kufurahishwa na elimu waliyoipata na kushukuru TBS kwa kuja kutoa elimu hiyo ambayo itawapa matokeo yenye tija kwenye shughuli zao za uzalishaji.Semina hii ilifanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime

Kampeni hii inaendelea Wilaya ya Nyamagana .

 TBS ikiendelea na kampeni ya elimu kwa umma katika shule ya msingi Nyamisangura na Shule ya sekondari Sirari Wilayani Tarime.
 Afisa Udhibiti Ubora,Mhandisi Paul Ndege akiwaelekeza wajasiriamali  utaratibu  wa kupata leseni ya ubora ya TBS bila gharama yoyote,katika semina iliyofanyika ukumbi wa Halmashauri Wilayani Tarime.
 Pichani ni Mhandisi Paul Ndege, Afisa Uthibiti Ubora akitoa somo kwa mjasiliamali kuhusu umuhimu wa kuuza bidhaa zilizothibitishwa na TBS
Mhandisi Paul Ndege akiendelea na semina ya Elimu kwa Umma juu ya kutambua Bidhaa hafifu Mjini Mara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...