Kampuni ya Mafuta ya TOTAL, imepunguza bei ya mafuta ya  TOTAL EXCELLIUM  kwa kutoa punguzo la TZS 70 kwa kila lita ya mafuta, muda wa siku tatu, kuanzia tarehe 13/02/2019 mpaka 15/02/2019 katika baadhi ya vituo vya TOTAL vilivyopo Dar es Salaam, Dodoma, Arusha, Moshi, Mwanza Mbeya na Morogoro
Taarifa hiyo imetolewa na Network Operations Manager wa vituo vya TOTAL, William Fillet, amesema uamuzi huo wa kupunguza bei ya mafuta ya TOTAL EXCELLIUM katika baadhi ya vituo vya TOTAL ni ili kuwapatia zawadi ya sikukuu ya wapendanao ya Valentine wateja wao, kwa kuonyesha ishara ya upendo na kuwawezesha kusherehekea sikukuu ya Valentine kwa Upendo.
Mkurugenzi wa Sheria na Uhusiano wa TOTAL, Marsha Msuya Kileo, amesema sambamba na punguzo hilo la bei kwenye mafuta, pia wateja wote wa watakaonunua chochote kwenye maduka ya Café Bonjour, yaliyoko kwenye vituo Total vilivyochaguliwa, watapatiwa zawadi ya maua ya Valentine kuonyesha upendo.
Marsha amesema, punguzo hilo, lenye kauli mbiu ya “Fill Up With Love”, yaani jaza mafuta kwa mapenzi. Marsha amewakumbusha watanzania, kuwa ukijaza mafuta kwenye kituo cha TOTAL, haujazi mafuta tuu, bali unajaza mafuta ya TOTAL EXCELLIUM yenye viambata vya kuifanya gari yako itumie mafuta kidogo na kwenda umbali mrefu, huku mafuta hayo yakiboresha injini ya gari yako.
Jumla ya vituo  vya TOTAL 16 vimeteuliwa kuendesha zoezi hilo, katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Arusha, Moshi, Mwanza Mbeya na Morogoro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...