Miongoni mwa wananchi hao ni George Miyango mkazi wa Buyekera mjini Bukoba ambaye katika mazungumzo na Nicolas Ngaiza wa Radio washirika Kasibante FM anaanza kwa kuelezea ufahamu wake kuhusu radio.

“Mimi ninavyofahamu redio ni kitovu cha mawasiliano makubwa na kuweza kupeleka habari kwa muda mfupi tofauti na ule upelekaji wa habari uliokuwepo, taarifa moja inaweza kuwafikia watu maelfu na maelfu kwa muda mfupi kuliko iliyokuwa inapeleka habari kwa farasi, kwa magari au kwa njia ya kupeleka vifurushi.”

Alipoulizwa kuwa radio inamsaidia vipi, Bwana Miyango amesema, “inanisaidia kupata habari za kijamii, kiuchumi na habari hata za vifo na vitu vingine ambavyo ninaweza kuwa sivielewi. Ninasikiliza redio hata nikiwa kwenye shughuli zangu na ninakuwa na redio.”

Hata hivyo amesema kuna changamoto kwenye kupata maudhui sahihi kwenye redio kwa sababu baadhi ya redio zina muegemeo mmoja au wa upande fulani kutokana na msimamo wa mmiliki wa radio.

Kwa mantiki hiyo amesema ni vyema wamiliki wa vyombo vya habari wasiegemee upande wowote na mamlaka zihakikishwe waandishi wa habari wako huru.

Amesihi watu wasio na hulka ya kusikiliza redio wabadili mitazamo yao na kuanza kusikiliza redio kwa sababu “maarifa yanatafutwa, unaposoma ukisaidiana na magazeti na redio ndipo unakuwa kama unanoa maarifa yako na unaweza kuwa mwanajamii bora na mwenye maarifa.”

HABARI KWA HISANI YA https://news.un.org/sw/

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...