Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe

Constantine Kanyasu ametaka ujenzi wa majengo ya Wizara mbalimbali yanayojengwa katika eneo la Ihumwa yajikite kutumia vyuma badala ya kutumia mbao ngumu ambapo kwa sasa Wizara ipo kwenye kampeni kubwa ya kuzuia matumizi ya miti hiyo ambayo ipo hatarini kutoweka

Amesema Wizara kwa sasa imepiga marufuku ukataji na usafirishaji wa magogo yanayozalisha mbao ngumu.Hayo yamesemwa na Naibu Waziri huyo wakati alipotembelea eneo hilo kwa ajili ya kukagua hatua za ujenzi wa jengo hilo unaoendelea jijini Dodoma.

Amesema endapo majengo ya Wizara zote yatatumia mbao za aina hizo zaidi ya magogo ya miti 300 itakatwa.

Aidha, Mhe.Kanyasu ameshauri Jengo la Wizara hiyo lisitumie nguzo za mbao kwa upande wa mbele katika sehemu ya kuingilia kama inavyoonekana kwenye ramani badala yake itumie nguzo za zege ili iweze kudumu kwa muda mrefu.

Pia, Mhe.Constantine Kanyasu ametaka timu ya wataalam mbalimbali ifanye kazi kwa pamoja katika hatua za mwisho za ukamilishaji wa jengo hilo la Wizara katika mji wa Kiserikali wa Ihumwa.

Amesema licha ya kuwa hatua ya ujenzi wa jengo hilo ni ya kuridhisha ila ametaka nguvu ziongezwe ili kuweza kulikamilisha jengo hilo ndani ya muda wa wiki mbili zijazo licha ya kuwa muda uliotolewa na Waziri Mkuu, Mhe.Kassim Majaliwa tayari umeshapita.

Katika nyingine, Mhe Kanyasu ameshauri hatua za kupanda miti pamoja kuandaa bustani za maua zianze mapema katika jengo hilo ili likishakamilika liwe kwenye madhari nzuri badala ya kusubili hadi pale jengo litakapokamilika kabisa

Kwa upande wake, Mkandarasi wa Suma JKT, Clement Shaibu amemueleza Naibu huyo kuwa ujenzi unaendelea vizuri na wanatarajia kukamilisha ndani ya wiki mbili zijazo.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiwa pamoja Wakandarasi akikagua jengo la Wizara ya Maliasili na Utalii wakati alipotembelea eneo la Ihumwa jijini Dodoma. 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akioneshwa mtindo wa paa kwa ndani utakavyokuwa katika jengo la Wizara ya Maliasili na Utalii na Mkandarasi Clement Shaibu wakati alipotembelea kwa ajili ya kukagua jengo hilo linalojengwa Ihumwa jijini Dodoma
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiwa pamoja Wakandarasi akikagua jengo la Wizara ya Maliasili na Utalii kwa ndani wakati alipotembelea eneo la Ihumwa jijini Dodoma.
Muonekano wa jengo la Wizara ya Maliasili na Utalii katika hatua za mwisho wa kukamilika kwake katika mji wa kiserikali wa Ihumwa jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii (katikati) akiwa na Mkandarasi pamoja na Katibu wake, Zulu Ngondya (kulia) wakiangalia baadhi ya ramani ya jengo la Wizara hiyo mara baada itakapokamilika.(PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...