NJOMBE 

Ikiwa siku moja imepita tangu naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi amuagize IGP Siro kutuma kikosi maalumu cha kiintelinsia kuongeza nguvu katika uchunguzi wa watekaji na wauaji wilayani Njombe , Hatimae hii leo kikosi hicho kimewasili mkoani Njombe kikiongozwa na Kamisha wa operesheni na mafunzo wa jeshi la polisi nchini Nsato Marijani. 

Akizungumza katika mkutano wa dharura na wananchi katika kituo kikuu cha mabasi mkoani Njombe mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka wakati akitamburisha kikosi hicho kilichosheheni wataalamu mbalimbali kutoka vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama nchini amewataka wananchi kutoa ushirikiano ili kuwabaini wahusika wamaovu hayo huku akidai hakuna mtu atakae achwa salama kama amehusika na mauaji. 

Katika mkutano huo pia Olesendeka amemuagiza kamanda wa polisi mkoa wa Njombe RPC Rennata Mzinga kumkamata mara moja aliyekuwa mratibu wa tiba mbadala na asilia mkoa wa Njombe Matias Gambishi ambaye pia ni afisa afya wa mkoa huo baada ya kulalamikiwa na waganga wataalamu wa tiba asili na mbadala kuwa amekuwa chanzo cha kusababisha migogoro katika chama chao pamoja kufanya usajiri holela wa waganga hao. 

Nae kamanda wa kikosi hicho maalumu Nsato Marijani ambaye Kamisha wa operesheni na mafunzo wa jeshi la polisi nchini anapata wasaha wa kuzungumza na wananchi ambapo anasema kikosi hicho kimekuja kwa kazi ya kuwasaka wahusika wa mauaji na kwamba kitawasaka popote walipo kwa heri ama shari. 

Kwa upande wananchi wanapongeza serikali kwa kuchukua hatua za haraka za kukabiliana na vitendo hivyo vya ukatili dhidi ya watoto.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...