Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Susan Mlawi
(Katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dodoma kuhusu Kikao Kazi
cha Maafisa Utamaduni wa Mikoa na Halmashauri zote Nchini kitakachofanyika
tarehe 27-28 Februari 2019 Jijini hapo.Kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya
Maendeleo ya Utamaduni wa Wizara hiyo Bw.Bonoface Kadili, na Kushoto ni
Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Kikao hicho Bw.Francis Songoro.
Na Shamimu Nyaki –WHUSM.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Susan Mlawi
ametoa wito kwa Maafisa Utamaduni wa Mikoa na Halmashauri nchini kushiriki kwa
wingi katika kikao kazi cha sekta hiyo kitakachofanyika kuanzi tarehe 27 na 28
Februari 2019 Jijini Dodoma.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dodoma, Mlawi ameeleza
kuwa kikao hicho ni cha 11 kufanyika ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni “Umoja
Upendo na Kazi :Asili ya Utamaduni Wetu” lengo ikiwa ni kuendeleza Sekta ya
Utamaduni hapa nchini.
“Lengo la kikao kazi hichi ni kuweka mikakati ya pamoja katika kutekeleza Sera ya
Utamaduni kwa ngazi ya Mikoa na Halmashauri pamoja na kuhamasisha ukuzaji na
matumizi sahihi ya lugha ya Kiswahili ambayo ndio lugha inayotambulisha nchi
yetu”. Alisema.
Ameongeza kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa kikao kazi hicho anatarajiwa
kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison
Mwakyembe huku kikifungwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa, Selemani Jaffo.
Aidha Mlawi amezitaja mada zitakazowasilishwa katika kikao kazi hicho
ambazo ni Ubidhaishaji wa Lugha ya Kiswahili,Utendaji kazi Kimuundo baina ya
Maafisa Utamaduni wa Wizara Mikoa na Halmashauri,Uhuishaji wa Sera ya Taifa
ya Utamaduni,Fursa za Utalii wa Kiutamaduni nchini.
Mada nyingine ni Ufahamu Kuhusu Haki Miliki na Hakishiriki za Wasanii,Fursa ya
Soko kwa Bidhaa za Utamaduni pamoja na Mada itakayohusu Umuhimu wa Sekta
ya Filamu katika kuimarisha Asili na Utamaduni wetu.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Susan
Mlawi (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini
Dodoma kuhusu Kikao Kazi cha Maafisa Utamaduni wa Mikoa na Halmashauri zote
Nchini kitakachofanyika tarehe 27-28 Februari 2019 Jijini hapo. Kulia kwake ni
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Utamaduni wa Wizara hiyo Bonoface
Kadili, na Kushoto ni Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Kikao hicho Bw.Francis
Songoro.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Utamaduni wa Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Bonoface Kadili akimkaribisha Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo Bibi.Susan Mlawi (Katikati) azungumze na waandishi wa habari leo
Jijini Dodoma kuhusu Kikao Kazi cha Maafisa Utamaduni wa Mikoa na Halmashauri
zote Nchini kitakachofanyika tarehe 27-28 Februari 2019 Jijini hapo. Kushoto ni
Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Kikao hicho Bw.Francis Songoro.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...