Bei za mafuta yanayopitia bandari ya Dar es Salaam zimepungua kwa mwezi wa pili mfululizo na kufikia shilingi 2,120 kwa lita moja ya petroli, 2,080 kwa dizeli na 2,046 kwa mafuta ya taa. 

Kwa kila lita kumekuwa na punguzo la shilingi 175 kwa petroli, shilingi 144 kwa dizeli na shilingi 156 kwa mafuta ya taa, kwa mujibu wa taarifa ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nistahi na Maji (EWURA) iliyotolewa jana mjini Dodoma. Bei hizo zitaanza kutumika kesho tarehe 6 Februari, 2019. 

Hii ina maana pia kwamba kwa mwezi Januari na Februari 2019, bei za rejareja za Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa zimepungua kwa jumla ya Shilingi 316, Shilingi 356 na Shilingi 323, mtawalia.
Taarifa hiyo imeeleza pia kwamba bei za mafuta yaliyopitia bandari ya Tanga zitaendelea kuwa zile za mwezi uliopita kwa sababu hakukuwa na shehena mpya. 
Hali kadhalika, bei za mafuta yaliyopitia bandari ya Mtwara zitaendelea kuwa zile zile zilizotangazwa Januari 25 2019, ambapo petroli ilipungua kwa shilingi 271 na dizeli shilingi 221 kwa lita.    

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano, 
EWURA.  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...