Na. Saja Kigumbe
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina amesema serikali za Tanzania na Misri zimekubaliana kuanzishwa kwa kiwanda kikubwa cha nyama na mazao ya ngozi hapa nchini.
Waziri Mpina amebainisha hayo jana Februari 5,2019 ofisini kwake jijini Dodoma mara baada ya kupata ugeni kutoka nchini Misri ukiongozwa na Waziri wa Kilimo wa nchi hiyo Prof. Ezzaldin Aboussteit.
“Tunaenda kujenga kiwanda kikubwa cha kusindika nyama, cha kusindika ngozi, cha kusindika mazao ya ngozi, kiwanda ambacho hakipo katika nchi hizi zote za Afrika ya Mashariki na Kati.” Alisema Mhe. Mpina
Waziri Mpina amemuhakikishia waziri huyo wa Misri kuwa rasilimali za mifugo na uvuvi zilizopo nchini zipo salama na kwamba wizara imekuwa ikifanya jitahada kuhakikisha samaki hawavuliwi kwa njia haramu na hakuna biashara haramu ili kuhakikisha rasilimali hizo zinanufaisha viwanda vya ndani na wawekezaji watakaokuja kuwekeza katika sekta hizo.
Aidha Waziri Mpina amemuarifu Waziri wa Kilimo wa Misri Prof. Ezzaldin Aboussteit kuwa hakuna mifugo inayoruhusiwa kuingia nchini kutoka nje ya nchi bila ya kuwa na vibali na kuwa usimamizi wa nchi katika rasilimali za mifugo na uvuvi uko salama.
Katika kikao hicho kilichoongozwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina, kilihudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega, makatibu wakuu wa wizara hiyo pamoja na manejimenti ya wizara.
Waziri wa Kilimo wa Misri Prof. Ezzaldin Aboussteit (kulia) akifafanua jambo katika kikao hicho huku akisiskilizwa kwa makini na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallaha Ulega na wajumbe wengine hawapo pichani
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina (wa tatu kushoto) akizungumza ofisini kwake baada ya kutembelewa na ujumbe kutoka Misri ukiongozwa na Waziri wa Kilimo wa nchi hiyo Prof. Ezzaldin Aboussteit
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...