Daktari bingwa wa Upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu MOI Dkt Nicephorus Rutabasibwa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika kambi ya upasuaji iliyofanywa kwa ushirikiano kati ya MOI na Hospitali ya Peking ya China
 Kiongozi wa jopo la madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Peking ya China Profesa Yuanli Zhao akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika kambi ya upasuaji iliyoendeshwa kwa ushirikiano kati ya MOI na hospitali ya Peking
Madaktari bingwa wa MOI pamoja na Peking ya China wakishiriki katika moja ya upasuaji wa kuondoa uvimbe kwenye ubongo kwa kutumia darubini ya kisasa. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)



NA KHAMISI MUSSA.

Madaktari Bingwa wa upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya fahamu leo wameshirikiana na madaktari Bingwa kutoka Hospitali ya Kimataifa ya Chuo Kikuu cha Peking cha nchini China kufanya upasuaji mkubwa wa kuondoa uvimbe kwenye Ubongo, upasuaji wa kuviba mishipa ya damu iliyopasuka kwenye ubongo pamoja na upasuaji wa mgongo

Upasuaji huu umefuatia ujio wa jopo la madaktari bingwa watatu wa upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya fahamu kutoka Hospitali ya chuo Kikuu cha Peking cha china ambao walipokelewa MOI tarehe 23/02/2019.

Akizungumza katika chumba cha Upasuaji MOI, Dkt Nicephorus Rutabansibwa amesema ushirikiano kati ya MOI na Peking utakuwa wenye manufaa makubwa kwani huduma za MOI zitaendelea kuwa bora na watanzania wataendelea kupata huduma hizo hapa nchini billa ya kwenda nje ya nchi.

“huu ni muendelezo wa ushirikiano tulioingia na wenzetu hawa wa Peking mwaka jana, tunaamini tutabadilishana uzoefu na wenzetu hawa ambao wamepiga hatua kubwa kwenye teknolojia ya matibabu, kupitaia ushirikiano huu mbinu tunazopata zitatusaidia kuendelea kutoa tiba bora na kwa wakati kwa wagonjwa wetu” alisema Dkt Rutabansibwa

Dkt Rutabansibwa amesema leo watawafanyia upasuaji wagonjwa 3 mmoja atafanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe kwenye ubongo kwa kutumia darubini ya kisasa, mwingine upasuaji wa mgongo na mwingine atafanyiwa upasuaji wa kuziba mishipa ya damu iliyopasuka kwenye kichwa.

Pia amesema ujio huu wa wataalamu kutoka peking umelenga kuweka mazingira bora ya ushirikiano na MOI ili watakapo kuja tena wajue ni maeneo gani yanahitaji kuwa kipaumbele kwenye ushirikiano.

Kwa upande wake kiongozi wa jopo la madaktari bingwa kutoka Peking Peking amesema ushirikiano kati ya MOI na Peking utakuwa wenye mafanikio makubwa na utawanufaisha wagonjwa pamoja na madaktari vijana ambao watapata fursa ya kusoma kenye chuo chao

“Tumefarijika kuja Tanzania, tumewaeleza hali halisi ya hospitali yet una vifaa tulivyonavyo, tunaamini kupitia ushirikiano huu wataalamu wa hapa watajifunza na pia tutatoa fursa kwa wataalamu 2- 3 kuja kujifunza kwetu” Alisema Profesa Zhao.

Kambi hii ni sehemu ya muendelezo wa mkataba wa ushirikiano uliosainiwa kati ya MOI, Chuo Kikuu cha MUHAS na Hospitali ya Peking ya China ambao umejikita katika ,Mafunzo ya muda mrefu na Mfupi, utafiti,tiba pamoja na uboreshaji wa miundombinu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...