Na Khadija Seif,Globu ya Jamii

MSANII wa tasnia ya filamu nchini Madebe Lidai amesema kuibuka  mshindi wa tuzo ya mchekeshaji bora wa mwaka sio yeye ndio bora kwani wachekeshaji wengi na wana majina katika fani hiyo.

Kumekuwa na minong'ono mingi   juu Madebe kuibuka mshindi katika tuzo ya wa uchekeshaji bora kwa mwaka jana.

 Madebe amesema kuwa kupewa tuzo hiyo aliokuwa  akishindanishwa na Msanii Mohammed a.k.a Mau Mafundi pamoja na Hassan Kazoa amesema haya kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram.

"Kikubwa ni kwamba mimi sio mchekeshaji ila nilithubutu kufanya uchekeshaji katika filamu yangu ya  Mama mwali ili kuonesha utofauti katika sanaa niliyonayo ambapo  leo nimeshinda sina maneno mengi namshukuru Mungu na wenzangu wasikate tamaa," amesema Lidai

Hata hivyo amewaomba radhi mashabiki zake kwa kilichotokea na kusema anasubiri uchambuzi wa Pofesa  Martine Mhando ili aweze kufanya ufafanuzi kupitia uchambuzi huo.

Pia ametoa wito wakati wa kupokea tuzo hiyo kwa wasanii wa kibongo kuona tuzo hiyo kama chachu ya kutengeneza kazi nzuri zenye manufaa Kwa taifa kwa ujumla na zenye mafundisho kwa jamii kwani mambo yapo mengi katika tunayoishi na kuacha.

"Tutambue nafasi  tulionayo ni kubwa hivyo lazima tuitumie katika kuelimisha jamii kwani matatizo yaliyopo wasanii yanatuhusu kupaza sauti zetu katika kujenga"amesema Madebe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...