Uongozi
wa Jimbo la Mahonda umejikita kuimarisha Sekta ya Michezo katika azma
nzima ya kuinua kiwango cha Michezo kitakachowawezesha Vijana ndani ya
Jimbo hilo kujiwekea njia ya kupata ajira kupitia fani hiyo muhimu kwa
sasa hapa Duniani.
Mke wa Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Mama Asha Suleiman Iddi amesema hayo baada ya kushuhudia pambano la kirafiki la Mchezo wa Mpira wa Pete {Netball} uliozikutanisha Timu za Madada wa Fujoni dhidi ya Kitope lililofanyika katika uwanja wa mahonda Kiwandani.
Mama Asha amesema utaratibu wa kuwapatia vifaa katika Michezo tofauti Vijana wa Jimbo hilo utaendelea ili kuwajengea ari ya kupenda Michezo licha ya kuimarisha Afya bora zitakazowaepusha na Maradhi mbali mbali pamoja na kuwa mbali na vikundi vya kihuni.
Amewataka Vijana hao kujikita katika masuala ya Kijamii na kuacha kasumba na mambo yanayoendelea kuenezwa na Watu walioshindwa kutafuta masuala ya msingi yatakayowawezesha Vijana hao kujitegemea zaidi.
Katika pambano hilo mbali ya kutafuta Timu ya Kombaini ya Netball ya Jimbo la Mahonda lakini pia ulikwenda sambamba na shamra shamra za maadhimisho ya Sherehe za kutimia Miaka 42 ya Chama cha Mapinduzi tokea kilipoasisiwa kwenye Uwanja wa Amani Mjini Zanzibar mnamo Mwaka 1977.
Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR)
Febuari 05, 2019

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...