*Asema wamebeba kundi kubwa katika jamii ambalo linawasikiliza, linawahusudu
*Awaomba waibadilishe jamii ili iachane na dawa za kulevya, atoa neno kwa jamii 


Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

MAKAMU wa Raia Samia Suluhu Hassan amesema wasanii ni muhimu sana katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya nchini kwani nyuma yao wamebeba kundi kubwa katika jamii ambalo liwasikiliza , linawafuatilia, linawahusudu na linawaamini, hivyo wanaouwezo wa kubadilisha jamii kuachana na dawa za kulevya ambazo madhara yake ni makubwa kwa Taifa.

Hata hivyo imeelezwa kwa sasa Serikali imefanikiwa kudhibiti kwa kiasi kikubwa uingiaji wa dawa za kulevya na takwimu zinaonesha wamedhibiti kwa asilimia 90 , hivyo imebakia asilimia 10 ambapo imewaomba watanzania kushiriki katika kukomesha dawa za kulenya nchini.


Akizungumza na wasanii kwenye kongamano la wasanii kujadili athari za dawa za kulevya lililofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalim Nyerere jijini Dar es Salaam Mama 

Samia amesema tatizo la matumizi haramu ya dawa za kulevya duniani ni kubwa na linazidi kuongezeka siku hadi siku. Idadi ya watumiaji na waathirika wa dawa za kulevya inazidi kuongezeka 
hapa nchini na wasanii ni moja kati ya makundi ambayo yameathirika zaidi na janga hilo.

"Hivi sasa watumiaji wanapatikana maeneo yote si mjini tu bali hata vijijini na la kusikitisha zaidi matumizi hayo sasa yameanza kujitokeza miongoni mwa wasanii wengi nchini.Jambo la kuumiza zaidi hata baadhi ya watoto wanaonekana kutumia dawa za kulevya .Watoto wetu wako katika hatari kubwa ya kutumbukia kwenye janga hili , hii ni kutokana na ukweli hawana uwezo wa kujilinda na hawajui namna ya kukabiliana na janga hili.Mara nyingi wamekuwa wakirubuniwa na kujikuta wametumbukia kwenye lindi la matumizi ya dawa hizo hatari,"amesema Mama Samia.

Ameongeza matumizi ya dawa za kulevya yana madhara mengi kiuchumi, kisiasa, mazingira ,kiafya na kijamii na kusisitiza pia hudhoofisha afya za watumiaji na kuathiri uwezo wao wa kufanya kazi na kwa upande wa afya husababisha magonjwa yakiwemo ya akili, homa ya ini , kifua kikuu , moyo na kuenea kwa kifua kikuu sugu.

"Nimefurahishwa kuwa kongamano hili linalenga katika kuangalia na kujadili namna ya kukabiliana na kutatua kwa pamoja tatizo la dawa za kulevya nchini hasa katika kundi la wasanii na katika jamii kwa ujumla.Tunafahamu dawa za kulevya vilevile zimechangia kwa kiasi kikubwa mmomonyoko wa maadili,hivyo ni matarajio yangu mtaangalia kwa kina tatizo la mmomonyo huo kwa wasanii na jamii kwa ujumla kutokana na matumizi ya dawa za kulevya,"amesema.

Wakati huo huo Mama Samia amesema amefurahishwa na taarifa za kukamatwa kwa dawa mbalimbali na kusababisha kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria watuhumiwa 4,602.Ameviomba vyombo vya sheria kuhakikisha wote wanaopatikana na hatia wanapewa adhabu kali ili fundisho kwa wengine.

Ameishauri Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya pamoja na kuanzisha vituo sita vya huduma ya methadone ambapo kwa ujumla waathirika 6300 wametibiwa lakini kuna waraibu wengi zaidi ambao hawajafikiwa, hivyo bajeti yao ikiruhusu vituo vijengwe nchi nzima kwa kuanza na maeneo yenye waaathirika wengi.

"Ila ni vema mkawekeza kwenye kutoa elimu zaidi kuhusu madhara ya dawa za kulevya kwa vijana na jamii kwa ujumla kuliko kujenga vituo kwa kuwa waswahili husema kinga ni bora kuliko tiba.Kuhusu utoaji wa elimu kwa jamii na hasa vijana niwaombe muwatumie wasanii.Pia wanangu wasanii ninyi muwe mfano bora kwa jamii kwa kuhakikisha mbali na maisha ya sanaa , maisha yenu halisi yaendane na majukumu yenu ya kuwa kioo chetu,"amesema.



Kuhusu changamoto ya matumizi mabaya ya dawa za hospitali zenye asili ya kulevya amepata taarifa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto imeshapeleka taarifa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) na Pharma Council ili waje na muongozo wa namna ya kudhibiti dawa 


hizo kuanzia inavyoingizwa nchini mpaka kwa mtumiaji wa mwisho.

Pia amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuzidisha misako kwenye maeneo yote hasa mipakani na bandari bubu na kwamba hawalifu wa dawa za kulevya wanambinu nyingi , hivyo ni vema maofisa wa uhamiaji wakajengewa uwezo ili kuhakikisha mipaka ya nchi inakuwa salama.

Kwa upande wake Kamishna wa Kinga na Tiba wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Dk.Peter Mfisi pamoja na kueleza kwa kina athari za matumizi ya dawa hizo amesema mamlaka chini ya uongozi wa Kamishina General Roger Sianga wamefanikiwa kudhibiti uingizwaji wa dawa kwa asilimia 90.

"Tunapambana na asilimia 10 ambayo imebakia na tayari tumeweka mikakati ya kukabiliana na wafayabishara wa dawa za kulevya , wanatumia njia ya Kusini kwa maana dawa chache ambazo zinaingizwa nchini zinatoke katika nchi ya Msumbiji.Kwetu tutaendelea na mapambano na sehemu 
kubwa ya wafanyabiashara hiyo wako magerezani na wengine wamekimbia nchini na wale wachache waliopo tunaendelea kuwasaka na kuwabaini,"amesema Dk.Mfisi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wasanii wa fani mbali mbali waliohudhuria  Kongamano Kuhusu Tatizo la Dawa za Kulevya kwa Wasanii lililoandaliwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo leo februari 13, 2019 lililofanyika katika  Kituo cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...