Na Khadija Seif,Globu ya jamii

MSANII wa Mrisho Mpoto a.k.a Mjomba amewashauri wasanii nchini kutengeneza tungo zitakazofichua uovu huku akielezea furaha yake kutokana na nyimbo zake kukubalika hata kwa Rais Dk.John Magufuli.

Akizungumza na Michuzi Blog Mpoto amesema nyimbo nyingi kwa sasa zimejikita zaidi kwenye mapenzi, na kusababisha wasanii wengi kuonekana ni wa aina moja.

Aidha ameeleza si kufanana kwa tungo tu bali pia hata miondoko ya uimbaji imekua ya kufanana sana kiasi kutokujua sauti ya nani pindi unaposikia wimbo kwenye redio.

Wakati huo huo Mpoto amesema amefurahishwa na juhudi za Rais Dk.John Magufuli kwa kuwa shabiki wa kazi zake kutokana na ustadi wa mashairi yake jinsi anavyomkumbusha baadhi ya mazuri pamoja na maovu yanayoendelea katika jamii.

"Sitegemei kutoa ngoma kwa sasa kutokana na wimbo wa Sizonje unaendelea kufanya vizuri sana toka nilipouachia na muitikio umekua mkubwa hadi Rais Magufuli ameweza kung'amua baadhi ya mashairi yanazungumza nini na kueleza anamjua Sizonje" alisema Mpoto .

Kuhusu utunzi wa nyimbo zake,Mpoto amesema baadhi ya kazi huchukua siku,wiki,mwezi hadi mwaka huku akiangalia na kuzingatia sana hadhira inahitaji kusikia kipi kwani mashairi yake yanakusudia kuigusa jamii zote hasa wa hali ya chini .

Pia amesema mambo yanabadlika anaweza kwa mwaka huu mashabiki zake watamshuhudia akivaa viatu.

Ametoa mwito kwa wasanii kujitengenezea utambulisho wao wa kipekee kwa hadhira ili kusaidia kazi zisiibiwe na maharamia .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...