Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi, amesema, anaridhishwa sana na kasi ya ukamilishaji wa jengo la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu linalojengwa katika mji wa Kiserikali ulipo katika Kata ya Mitumba- Ihumwa nje kidogo ya Jiji la Dodoma
Jana ( Jumatano) Profesa Kilangi aliwoongoza Wakurugenzi, Wakurugenzi Wasaidizi na Wakuu wa Vitengo kukagua kazi inayoendelea katika ukamilishaji wa jengo hilo.
“Ninaridhishwa na ninafurahi sana kwa kasi na kazi nzuri ya ukamilishaji wa jengo hili. Kila ninapofika hapa kwenye site nakuta kazi mpya inaendelea, hongera sana Injinia kwa usimamizi wako pamoja na timu yako” amesema.
Akiogozwa na Injinia Suma Atupele. Mwanasheria Mkuu na ujumbe wake alipita na kukagua kila Ofisi huku akitoa maelekezo kwa Naibu Mwanasheria Mkuu na Mkurugenzi wa Utawala na Raslimali Watu juu ya mpangilio na mgawanyo wa Ofisi kwa kuzingatia muundo na majukumu ya Ofisi.
Katika maelekezo yake kwa viongozi hao, Profesa Kliangi amesisitiza katika upangaji wa Ofisi kuhakikisha kwamba, Wakurugenzi na Wakurugenzi Wasaidizi na maafisa walio chini yao hasa kutoka Divisheni za kisheria wanakuwa katika utaratibu wa kuhamia katika jengo hilo pale litakapokuwa tayari kuhamia.
Baada ya kukagua maendeleo ya ukamilishaji wa jengo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na timu yake alipata pia fursa ya kuangalia eneo zima lenye ukubwa wa ekari tano ambalo limetengwa kwa ajili ya ujenzi wa awamu ya pili wa Jengo kubwa zaidi ambalo litakuwa na uwezo wa kutosheleza watumishi wote wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu pamoja na matumizi mengine yakiwamo ya ujenzi wa Chuo maalum kitakachokuwa kikitoa mafunzo kwa Mawakili wa Serikali.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Kilangi akifafanua juu
ya mgawanyo wa Ofisi kwa baadhi ya wakurugenzi, wakurugenzi
wasaidizi na wakuu wa vitengo wakati walipotembelea kukagua maendeleo
ya kazi ya ukamilishwaji wa jengo la awamu ya kwanza la Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali linaojengwa katika Mji wa Kiserikali
katika Kata ya Mitumba- Ihumwa nje kidogo ya Jiji la Dodoma. Mwanasheria
Mkuu amesema anaridhishwa kasi ya kukamilishwa kwa kazi zilizobaki
katika jengo hilo
Injinia
Mwanadada Suma Atupele ambaye amekuwa akisimamia kazi za ujenzi wa
Jengo la Mwanasheria Mkuu wa Serikali, tangu jengo hilo lilipoanza
kujengwa akitoa maelezo kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na ujumbe wake
namna Ofisi zitakavyo fanyiwa mgawanyo ( partitioning).
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Kilangi akielezea kwa kuchora
ardhini mgawanyo na matumizi ya sehemu ya eneo la ukubwa wa ekari
karibu tano ikiwamo sehemu ambayo limejengwa jengo la awali ambalo
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu imepewa na Serikali katika Mji wa
Kiserikali Mitumba- Ihumwa.
Kazi ya uwekeaji wa (vigae)tiles ukiendelea, kama inavyoonekana katika chumba hiki.
Kazi ya upakaji rangi nje ya jengo ikiwa inaendelea kama inavyoonekana
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...