Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso akifungua maji kwenye mradi wa Ulonge alipofika kuukagua akiwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela mkoani Iringa.Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso ameipongeza Mamlaka ya Maji ya mjini Iringa (IRUWASA) kwa kazi nzuri inayofanya katika kutoa huduma ya majisafi kwa manispaa ya mji wa Iringa kwa asilimia 96.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Iringa (IRUWASA), Gilbert Kayange akiwaongoza Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela na Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso wakati wakikagua Chanzo cha Maji cha Ndyuka kinachohudumia wakazi wa Manispaa ya Mji wa Iringa, mkoani Iringa.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela (kushoto) akiteta na Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (katikati) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Iringa (IRUWASA), Gilbert Kayange katika Chanzo na Mtambo wa Kutibu Maji, Ndyuka.
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso akipokea maelezo kutoka Mhaidrolojia wa Bodi ya Maji ya Bonde la Mto Rufiji, David Munkyala pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela (kushoto) katika sehemu ya kupima wingi wa maji cha Ndyuka katika Mkoa wa Iringa.
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela wakati akikagua ujenzi wa ofisi za Bodi ya Bonde la Maji la Rufiji katika Manispaa ya Mji wa Iringa,mkoani Iringa.


Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso ameipongeza Mamlaka ya Maji ya mjini Iringa (IRUWASA) kwa kazi nzuri inayofanya katika kutoa huduma ya majisafi kwa manispaa ya mji wa Iringa kwa asilimia 96.

Naibu Waziri Aweso ametoa pongezi hizo wakati alipokua akizungumza na watumishi wa mamlaka hiyo mara baada ya kujionea miradi inayotekelezwa na mamlaka hiyo wakati alipokuwa katika ziara yake ya kikazi katika manispaa ya mji wa Iringa leo.

''IRUWASA ni moja ya mamlaka tunazojivunia kama wizara kutokana na kazi yenu nzuri na mimi binafsi nimejionea jambo hili kwa kufika hapa, hii inatokana na uongozi mzuri wa Mkuregenzi Mtendaji na Bodi yenu, pamoja na watumishi mlio nao'', amesema Aweso.

''Mmepiga hatua kubwa kiteknolojia kwa matumizi ya mita za kulipia kabla ya matumizi (prepaid meters, kukusanya madeni kutoka kwa wateja waliokuwa wadaiwa sugu, teknolojia ya ukusanyaji mapato na kuwaunganishia wateja wapya huduma miongoni kazi nzuri mnazozifanya'', amesema Aweso.

Aidha, Naibu Waziri Aweso ameitaka mamlaka hiyo kuongeza nguvu katika ujenzi wa mfumo wa majitaka ambao umefikia asilimia 40 na kufikisha huduma ya maji ya uhakika katika eneo la Nduli kwa kushirikiana na manispaa kwa kuwa bado huduma hiyo ni changamoto kwa wakazi wa eneo hilo.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa IRUWASA, Gilbert Kayange amesema mpaka sasa wameweza kufunga prepaid meters 1857 tangu mwaka 2016 na kupunguza madeni kwa taasisi za Serikali kwa asilimia 30.

Kayange ameongeza kuwa wameweza kupunguza tatizo la upotevu wa maji mpaka kufikia asilimia 24.5 na wamejipanga kufanikisha zoezi la kupeleka maji katika eneo la Nduli kwa lengo la kufikisha asilimia 100 ya huduma ya maji kwa manispaa hiyo.

IRUWASA imekuwa ni mamlaka ya mfano kwa upande wa matumizi ya prepaid meters kwa mafanikio na immekuwa ni sehemu ya mamlaka nyingine za maji nchini katika kujifunza kuhusiana na matumizi ya mita hizo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...