Naibu Waziri wa
Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati) akikabidhi
kompyuta kwa Mbunge wa Mpanda Mjini, Sebastian Kapufi (wa pili kulia) kwa ajili
ya shule za sekondari mjini humo. Wakishuhudia, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi
wa Uendeshaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Mhandisi Albert Richard na
Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi, Abdallah Malela (wa pili kushoto)
Naibu Waziri wa
Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akifafanua jambo kwa
viongozi wa Mkoa wa Katavi, Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda na waalimu wa
sekondari (hawapo pichani) kuhusu ukuaji na maendeleo wa sekta ya Mawasiliano
nchini. Kulia kwake ni Mbunge wa Mpanda Mjini, Mhe. Sebastian Kapufi na kushoto
ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi, Abdallah Malela
Mkurugenzi wa
Uendeshaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Mhandisi Albert Richard akitoa
maelezo ya kompyuta walizotoa kwa shule za sekondari za Mpanda. Walioketi
wakimsikiliza, wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano
Mhandisi Atashasta Nditiye na katikati ni
Mbunge wa Mpanda Mjini, Sebastian Kapufi
Afisa Elimu wa Shule
za Sekondari wa Manispaa ya Mpanda, Enelia Lutungulu akisoma risala ya shukrani
kwa Serikali kwa niaba ya waalimu na wanafunzi wa shule kwa kuzipatia shule
hizo kompyuta 25. Walioketi wakimsikiliza wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri wa
Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye na katikati ni Mbunge wa Mpanda Mjini, Sebastian
Kapufi
Waalimu wa shule za sekondari, viongozi na watendaji wa mkoa wa Katavi na Manispaa ya Mpanda wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (hayupo pichani) wakati akiwahutubia kabla ya kukabidhi kompyuta kwa ajili ya shule za sekondari za Mpanda
Naibu Waziri wa
Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akisisitiza jambo kwa Afisa
Usalama Msaidizi wa Uwanja wa Ndege wa Katavi, Fredrick Valentine(wa kwanza
kulia) wakati akikagua miundombinu na hali ya uwanja huo akiwa ziarani mkoani
humo. Mbunge wa Mpanda Mjini, Sebastian Kapufi (wa tatu kulia) akifuatilia kwa
makini mazungumzo hayo .
Naibu Waziri wa
Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (aliyesimama mbele amefunga
mikono) akiwa kwenye picha ya pamoja na waalimu wa shule za sekondari, viongozi
na watendaji wa mkoa wa Katavi na Manispaa ya Mpanda. Wan ne kulia ni Mbunge wa
Mpanda Mjini, Sebastian Kapufi na wa tano kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa
Katavi, Abdallah Malela


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...