Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimjulia hali Mbunge wa
Misungwi,Charles Kitwanga ambaye amelazwa katika Hospitali ya Muhimbili
jijini Dar es salaam kwa matibabu.Picha na IKULU.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 02
Februari, 2019 amemjulia hali Mbunge wa Jimbo la Misungwi Mhe. Charles Kitwanga
ambaye amelazwa katika wodi ya Mwaisela katika Hospitali ya Taifa Muhimbili
Jijini Dar es Salaam kwa matibabu.
Mhe.
Kitwanga alilazwa hospitalini hapo tangu tarehe 31 Januari, 2019.
Mkuu wa
Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali Dkt. Juma Mfinanga amemueleza Mhe. Rais
Magufuli kuwa hali ya Mhe. Kitwanga inaendelea vizuri ikilinganishwa na wakati
alipofika hospitalini hapo.
Akiwa
wodini hapo Mhe. Rais Magufuli ameshiriki sala ya kumuombea Mhe. Kitwanga ilia
pone haraka na amewashukuru Madaktari na Wauguzi kwa juhudi kubwa wanazozifanya
kuwahudumia wagonjwa.




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...