Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda katika kujali na kunusuru
kazi za Wasanii amewatafutia mkopo wa Shilingi Bilioni 2 bila riba
zitakazotolewa kwenye Halmashauri za Mkoa huo kupitia fungu la mkopo wa
10% zinazotolewa kwa Vijana, Walemavu na kinamama kwa lengo la
kuwawezesha wasanii kufanya kazi zao kwa ufanisi na kuziingiza sokoni.
RC Makonda amesema wasanii wengi wamejikuta wakizalisha kazi nzuri lakini wanakosa mitaji ya kuingiza kazi zao sokoni kutokana na kukosa mitaji jambo linalowapelekea wenye pesa kutumia fursa hiyo kunyonya kazi za wasanii na mwisho wa siku wanazidi kudidimia.
Aidha RC Makonda amesema hadi kufikia mwezi March 01 mkopo huo utakuwa tayari na ameshazielekeza halmashauri kutoa fedha hizo huku akiwasihi wasanii kuchangamkia fursa hiyo.
Hayo yote yamejiri wakati wa kikao baina ya RC Makonda na Wasanii kilicholenga kutatua kero za wasanii wa tasnia mbalombali.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...