Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha.
SHULE ya msingi Maendeleo ,kata ya Mailmoja Kibaha, mkoani Pwani, inakabiliwa na msongamano mkubwa wa wanafunzi ambapo darasa moja lina wanafunzi 284.
Changamoto hiyo aliitaja ,mwalimu mkuu wa shule hiyo Miriam Mkama wakati mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kata ya Maili Moja Mathayo Mkayala alipofanya ziara kutembelea miradi ya elimu na barabara akiwa na kamati ya siasa ya kata hiyo .
Alisema ,shule hiyo ina wanafunzi wengi ikiwemo wa awali wanafunzi 153, la kwanza wako 284 la pili wako 209, tatu wako 210, la nne wako 171, la tano wako 177, la sita wako 175, saba 158 na memkwa wako sita.
Alitaja changamoto nyingine ,ni upungufu wa vyoo ambapo wavulana 792 wanatumia vyoo vitano mapungufu 26 upande wa wasichana 756 wanatumia vyoo vinne .
Nae mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Maili Moja ,Mathayo Mkayala alisema ,kutokana na hali hiyo kuna kila sababu ya wananchi wa kata ya maili Moja kusaidia ujenzi wa madarasa mapya ili kupunguza msongamano huo ambao unahatarisha wanafunzi kutoweza kusoma vizuri.
"Wanafunzi wamejazana hata namna ya kufundishwa inakuwa ni ngumu hili ni tatizo hivyo wananchi wanapaswa kuliangalia suala hili kwa upekee kwa kujenga madarasa mengine,” alisema Mkayala.
Awali, diwani wa Kata ya Maili Moja ,Ramadhan Lutambi alisema ,changamoto ni kubwa na wameanza mchakato wa kuwaomba wazazi na wananchi kujitolea matofali matatu yamefika 980 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ambapo kwa sasa wameanza darasa moja linalojengwa na wananchi.





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...