NA MWAMVUA MWINYI, KISARAWE 

TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU)wilayani Kisarawe, Mkoani Pwani, imemfikisha mahakamani ofisa tawala wilayani humo, John Mwendamaka kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa ya sh. milioni mbili ikiwa ni kinyume na kifungu cha 15 (1)cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa na. 11/2007.

Ofisa huyo anadaiwa kuomba kiasi hicho, kutoka kwa mtoa taarifa ili aweze kumsaidia mdogo wake kujiunga na mafunzo ya Jeshi la kujenga Taifa. 

John Mwendamaka ambae alifunguliwa kesi ya jinai namba 22 ya mwaka 2019 ni ofisa tawala katika ofisi ya katibu tawala wa wilaya ya Kisarawe. 

Akisoma mashtaka hayo mbele ya hakimu mkazi wilaya ya Kisarawe Devotha Kisoka, mwendesha mashtaka TAKUKURU  Naftali  Mnzava, aliieleza mahakama kwamba mshtakiwa alitenda kosa la kuomba rushwa milioni mbili kwa ajili ya kumsaidia mdogo wa mtoa taarifa kujiunga na mafunzo ya jeshi. 

Aidha mshtakiwa, alikana makosa yote mawili na dhamana ilikuwa wazi hivyo alipata dhamana baada ya kutimiza masharti. 

Kesi hiyo itakuja kwa ajili ya hoja za awali march 5 mwaka huu. 

Hata hivyo,  kamanda wa TAKUKURU mkoani Pwani, Suzana Raymond aliiasa jamii kufuata taratibu, kanuni za sheria za nchi ili kwenda na kasi ya awamu ya tano, chini ya Rais Dkt. John Magufuli.

Pamoja na hayo ,Suzana alisema kuomba na kupokea rushwa ni kosa kisheria hivyo kila mmoja ajiepushe na vitendo hivyo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...