Na Said Mwishehe, Glob ya Jamii 

MUIGIZAJI maarufu nchini Steven  Mengere almaarufu Steve Nyerere amemuomba radhi msanii wa muziki wa Bongo fleva Omary Nyembo a.k.a Ommy Dimpozy.

Kwa kukumbusha Steve Nyerere alitoa kauli ya kwamba Ommy Dimpoz hawezi tena kutoa nyimbo yeyote kutokana na maradhi yanayomsumbua.

Hata hivyo msanii Ommy Dimpoz ameipua wimbo wake kabisa unaokwenda kwa jina la Ni wewe.Steve Nyerere baada ya Kutoka kwa wimbo huo amekuwa akishambuliwa na makundi ya watu mbalimbali mitandaoni .

Kupitia ukurasa wake wa Istagramu Steven Nyerere leo februari 9,2019 ameandika hivi ." kwanza nichukuwe fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu ,lakini pili nichukuwe fursa hii kumuomba radhi ndugu yangu Dimpoz kwa namna alivyopokea kauli yangu niliyoitoa dhidi yake na zaidi niwaombe radhi watanzania wote na wapenzi wa Sanaa .Binadamu unapoona hapa umekosea busara inatutaka kukiri kukosea nami nikiri kukosea kutokana na ile kauli yangu kwa Dimpoz.

" Lakini ifahamike kwamba kauli ile haikuwa kwamba namtakia mabaya Dimpoz hapana ila kwa tulivyokuwa tunapata taarifa kwakweli zilikuwa zinatukatisha tamaa," amesema Steve Nyerere.

Ameongeza kuwa mengi yameongelewa lakini ifahamike kwamba hakuwa na nia mbaya wala hakuwa na ugomvi na Dimpoz bali kama Binadamu hutokea kuteleza kwenye kuzungumza na hivyo asichukuliwe kwaniambaya .

"Lakini tunafahamu kwamba Mwenyezi Mungu hufanya miujiza yake kutokana na sababu furani hivyo miujiza ya kumuinua ndugu yetu na kurudi kwenye kazi zake imetokana na imani aliyonayo Dimpoz kwa muumba wake.

" Najua mie niliteleza kwa kusema kwamba Dimpoz hatoimba tena lakini sikuwa na nia hiyo ,kwangu natamani Dimpoz asiimbe tena Hapana kutokana na vichekesho mbalimbali vinavyotolewa juu yangu lakini vinanifurahisha kwani vinazidi kuupaisha wimbo mpya wa Ni wewe. 

"Naomba kuchukua fursa hii kuwaomba watanzania na wapenzi wa
Muziki kuzidi kumsapoti ndugu yetu pamoja na Kumuombea dua kwa Mwenyezi Mungu ili azidi kuimarika kiafya."amesema Steven Nyerere.
Ikumbukwe kuwa Ommy Dimpoz kwa muda mrefu amekuwa kimya katika muziki kutokana na kusumbuliwa na tatizo la koo ambapo alilazimika kwenda nje ya nchi kwa matibabu .

Hata hivyo kwasasa afya yake imeimarika na tayari ametoa wimbo mpya wa Ni wewe ambao umeaza kukubalika na kupendwa na wapenzi wa muziki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...