Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii

Tamasha kubwa la Pasaka linalosubiriwa kwa hamu linatarajiwa kuanza kuwasha moto kwenye viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es Salaam, April 21, 2019.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar, Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama amesema tamasha hilo litakuwa la kihistoria kutokana na kuzunguka mikoa isiyopungua 10, amesema Mikoa hiyo itaongezwa kwa ajili yakutoa fursa kwa wengine kushuhudia burudani hiyo.

Msama amesema Mikoa ambayo imethibitishwa mpaka sasa kwa Wananchi kukaa mkao wa burudani ni Simiyu, Mwanza na Iringa ambayo imepitishwa na Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo.

‘’Wakazi wa Dar es Salaam na Mikoani mjiandae na Tamasha hili la Kihistoria, kuna Msanii mkubwa anatarajiwa kuhudhuria tamasha hili, si lakukosa’’, amesema Msama

Pia Msama amesema kuwa lengo kubwa kufanya Tamasha hilo ni kuombea Amani Taifa pamoja na Viongozi wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ambaye amefanya kazi kubwa na nzuri katika kipindi cha uongozi wake ndani ya miaka mitatu.

Kaulimbiu ya Tamasha hilo ni: Umoja na Upendo, hudumisha amani katika nchi.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari maandalizi ya tamasha la Pasaka linalosubiriwa kwa hamu,ambalo linatarajiwa kuanza kuwasha moto kwenye viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es Salaam, April 21, 2019. Msama amesema kuwa tamasha hilo litakuwa la kihistoria kutokana na kuzunguka mikoa isiyopungua 10, amesema Mikoa hiyo itaongezwa kwa ajili ya kutoa fursa kwa wengine kushuhudia burudani hiyo.

Baadhi ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Msama Promotions, Alex Msama alipokuwa akizungumza nao leo jijini Dar kuhusu muendelezo wa maandalizi ya tamasha la pasaka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...