Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit C.V Kakoko anasikitika kutangaza kifo cha Baba yake mzazi, Mzee Conatus Vitalis Kakoko (81) kilichotokea juzi katika Hospitali ya Agakhan alipokuwa amelazwa kwa takribani wiki moja akisumbuliwa na maradhi ya Ini na Figo.

Hadi umauti unamkuta, Mzee Conatus Vitalis Kakoko ameacha watoto wanne (4) na wajukuu kumi na tano (15).

Misa ya kumuaga marehemu Mzee Conatus Vitalis Kakoko itafanyika katika kanisa la MT. Petrol lililopo Oysterbay siku ya Jumatatu, tarehe 11/2/2019 saa tatu asubuhi.

Mara baada ya misa hiyo, mwili wa marehemu Mzee Conatus Vitalis Kakoko utasafirishwa, ambapo Mazishi yatafanyika  siku ya Jumatato tarehe 13/02/2019 kijijini kwake, Munjebwe, Rulenge mkoani.



Bwana Ametoa na Bwana Ametwaa. Jina lake litukuzwe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...