Na Agness  Francis,blogu ya Jamii.

KAMATI ya uchaguzi ya Shirikisho la soka Tanzania  (TFF)  imefunguka rasmi kuwa itatangaza tarehe ya uchaguzi wa klabu ya Yanga  ifikapo machi 5 mwaka huu,ni baada ya  kamati hiyo kukaa kimya kwa muda mrefu na kuleta sintofahamu kwa baadhi ya wanachama wa klabu hiyo iliyokita maskani yake Jangwani maeneo ya Kariakoo Jijini Dar Da Salaam. 

Amesema hayo  Mwenyekiti wa kamati  ya uchaguzi ya Shirikisho la soka Tanzania  (TFF)  Ally Mchunguhela  kuwa tayari ameshakutana na viongozi wa klabu ya Yanga  na kukubaliana  kuwa sasa  kinachosuburiwa ni kutangazwa kwa tarehe rasmi ya uchaguzi huo unaosubiriwa kwa hamu na wapenzi wa klabu hiyo.

Mchungahela amesema kuwa uchaguzi huo ulipaswa kufanyika januari 13 mwaka huu  lakini kutokana na  baadhi ya wanachama wa Yanga kufungua  kesi mahakamani kusimamisha mchakato huo  na kupelekea zoezi zima  la uchaguzi  kusimama.

;Uchaguzi wa Yanga  utafanyika na hakutakuwa tena na mchakato mwingine  mpya  bali utaendelea palepale  ulipokuwa umefikia ,na  ifikapo Tarehe 5 Machi tutatangaza rasmi tarehe  mpya ya uchaguzi wa  Yanga na naamini utafanyika;amesema mchungahela.

Aidha Mchungahela amesema kuwa  mpaka kufikia tarehe itakayotangazwa rasmi ya uchaguzi  huo kila kitu kitakwenda sawa na hakutakuwa tena na kizuizi kingine ambacho kitafanya mchakato mzima kusimama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...