Bi.
Marie Msellemu, Meneja Mawasiliano wa TPDC akimkabidhi hundi Mkuu wa
Mkoa wa Mtwara Mh. Bw. Gelasius Byakanwa kiasi cha Tsh,. 13, 258,042 kwa
ajili ya ujenzi wa madarasa Mkoani Mtwara.
Katika
jitihada za kutekeleza dhana ya uwajibikaji kwa jamii (CSR) Shirika la
Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limeendelea kutekeleza kwa vitendo
dhana hii kwa kushiriki katika kutekeleza miradi mbali mbali ya
maendeleo Mkoani Mtwara.
Katika
tukio la hivi karibuni, TPDC imeweza kumkabidhi Mkuu wa mkoa wa Mtwara,
Mh. Bw. Gelasius Byakanwa hundi ya kiasi cha shilingi milioni kumi na
tatu laki mbili hamsini elfu na arobaini na mbili ili kusaidia ujenzi wa
darasa moja katika halmashauri ya wilaya ya Mtwara.
Akiongea
katika tukio hilo, Mh. Byakanwa alisema TPDC imefanya jambo kubwa na
kuonyesha uzalendo kwa kurudisha kwa jamii, na aliishukuru TPDC kwa
kuendelea kushiriki katika kutatua changamoto mbalimbali mkoani Mtwara,
husani zile zinazoikumba sekta ya huduma za jamii ikiwemo elimu. Vile
vile mkuu wa mkoa alitoa rai kwa wadau na wawekezaji waliopo mkoani
Mtwara kuiga mfano wa TPDC katika kuwajali wananchi kwa kuchangia katika
shughuli mbalimbali za maendeleo.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mtwara Ndg.Omari Kipanga akitoa ufafanuzi wa mahitaji ya elimu mkoani Mtwara.
Akimkabidhi
mfano wa hundi kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara kwa niaba ya Mkurugenzi
Mtendaji wa TPDC Bi. Marie Msellemu ambaye ni Meneja Mawasiliano wa
Shirika alisema “TPDC ni mdau mkubwa wa Mkoa wa Mtwara, na kwa kupitia
mfuko wa uwajibikaji kwa jamii (CSR), TPDC imekuwa ikiwashika mkono
wananchi wa Mkoa wa Mtwara na mikoa ya jirani katika kuboresha huduma
za jamii kama vile elimu, afya, maji na hivyo kiasi hiki cha fedha
kitauwezesha mkoa kuendelea kufikia lengo la kuweka mazingira mazuri ya
kusomea kwa watoto wetu”.
Wakati
huo huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Ndg.
Omari Kipanga alieleza kuwa “Sisi kama halmashauri tumefarijika sana
kwa msaada huu uliotolewa na TPDC, kwani fedha hizi zitaelekezwa moja
kwa moja katika ujenzi wa madarasa katika halmashauri ya Wilaya yetu
kama ilivyokusudiwa. Mchango huu uliotolewa na TPDC unakwenda
kukamilisha kazi ya kuezeka madarasa manne katika shule ya msingi
Mitambo pamoja na madarasa mawili katika shule ya sekondari ya
Madimba’’.
Mkurugenzi
Kipanga aliendelea kusisitiza kwamba uhitaji bado ni mkubwa kuweza
kukamilisha uhitaji wa madarasa kwa Mkoa wa Mtwara na kuwataka wadau wa
elimu na wawekezaji mbalimbali waliopo mkoani Mtwara kuiga mfano wa TPDC
katika kurudisha kwa jamii na kuimarisha elimu mkoani hapo.
Meneja Mawasiliano wa TPDC Bi. Marie Msellemu akikabidhi hundi kwa mratibu wa taasis ya TAKUWA Bi. Hadija Malibecha
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Ndg. Evod Mmanda naye aliungana na
viongozi waliotangulia kwa kuishukuru na kuipongeza TPDC kwa kusaidia
kuboresha huduma mbali mbali za kijamii mkoani Mtwara. Alieleza kuwa “Si
mara ya kwanza kwa TPDC kuchangia kwani mwaka jana tumepokea kiasi cha
21,151,500 za kumalizia ujenzi wa zahanati ya kijjiji cha Mngoji pamoja
na kiasi cha 12,000,000 za ujenzi wa choo cha wanafunzi wenye uhitaji
maalumu katika shule ya msingi Shangani”.
Katika
hatua nyingine TPDC ilikabidhi Taasisi ya Kusaidia Wanawake Mkoani
Mtwara (TAKUWA) kiasi cha milioni tatu laki tisa na elfu sabini kwa
ajili ya unununuzi wa vitendea kazi vya ofisi ili kurahisisha shuguli za
kila siku za taasisi hiyo.
Mratibu
wa taasiis hiyo Bi. Hadija Malibecha alishukuru TPDC kwa msaada huo na
alieleza kuwa “kabla ya upatikanaji wa vifaa hivyo tulikua tunafanya
kazi katika mazingira magumu lakini sasa TPDC imetuboreshea mazingira ya
kazi na kazi zinaenda vizuri”.
TAKUWA inasaidia vikundi vya wanawake kwa ajili ya kuinua shughuli mbalimbali za kiuchumi na elimu. Jumla ya vikundi 12 vya wakinamama mkoani mtwara vinasimamiwa na taasisi hii katika kupewa mafunzo ya ujasiriamali kama kutengeneza sabuni, ufugaji wa nyuki na ufugaji wa wa mbuzi lengo ikiwa ni kuboresha maisha ya wanawake.
TAKUWA inasaidia vikundi vya wanawake kwa ajili ya kuinua shughuli mbalimbali za kiuchumi na elimu. Jumla ya vikundi 12 vya wakinamama mkoani mtwara vinasimamiwa na taasisi hii katika kupewa mafunzo ya ujasiriamali kama kutengeneza sabuni, ufugaji wa nyuki na ufugaji wa wa mbuzi lengo ikiwa ni kuboresha maisha ya wanawake.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...