Daktari
bingwa wa wagonjwa wa moyo waliolazwa katika chumba cha uangalizi
maalum (ICU) Vivian Mlawi akielezea namna chumba cha ICU
kinavyowahudumia wagonjwa waliotoka katika chumba cha upasuaji kwa
viongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya
Kinondoni walioongozana na Msichana wa kwanza kitaifa katika matokeo ya
kidato cha nne 2018 Maria Manyama walipotembelea taasisi hiyo leo Jijini
Dar es Salaam. 
Mkurugenzi
wa Idara ya Tiba Shirikishi na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo
Delila Kimambo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) akiongea jambo
na Msichana wa kwanza kitaifa katika matokeo ya kidato cha nne 2018
Maria Manyama mwenye ndoto ya kuwa daktari bingwa wa magonjwa ya moyo
alipotembelea taasisi hiyo pamoja na viongozi wa Umoja wa Vijana wa
Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Kinondoni leo Jijini Dar es Salaam
kwa ajili ya kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo zinazotolewa. 
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Agnes Kuhenga (wa pili kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Huduma ya Uuguzi Robert Mallya wakizungumza na Viongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Kinondoni walioongozana na Msichana wa kwanza kitaifa katika matokeo ya kidato cha nne 2018 Maria Manyama walipotembelea taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Agnes Kuhenga (wa pili kushoto) pamoja na viongozi wa taasisi hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Kinondoni baada ya kufanya ziara katika taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo ziara. Picha na JKCI .
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Agnes Kuhenga (wa pili kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Huduma ya Uuguzi Robert Mallya wakizungumza na Viongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Kinondoni walioongozana na Msichana wa kwanza kitaifa katika matokeo ya kidato cha nne 2018 Maria Manyama walipotembelea taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Agnes Kuhenga (wa pili kushoto) pamoja na viongozi wa taasisi hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Kinondoni baada ya kufanya ziara katika taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo ziara. Picha na JKCI .
UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), wameishauri Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), kufuatilia na kulea vipaji vya watoto wenye ndoto ya kuwa madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa siku zijazo.
Rai hiyo imetolewa hospitalini hapo leo na Katibu wa UVCCM Wilaya ya Kinondoni, Rashid Semindu, wakati walipofanya ziara wakiwa wameambatana na Maria Manyama ambaye ni msichana wa kwanza kitaifa katika matokeo ya kidato cha nne 2018 yaliyotangazwa hivi karibuni na Baraza la Mitihani la Taifa.
“Tunaipongeza serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya uongozi wa Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais, Dkt. John Pombe Magufuli, kwa uwekezaji mkubwa uliofanyika katika taasisi hii”.
“Tunawapongeza nanyi wafanyakazi wa Taasisi hii kwa kuendelea kufanya kazi kwa moyo mkubwa kusaidia watanzania na wagonjwa wengine ambao mmetueleza huwa wagonjwa wengine mnawapokea kutoka nje ya nchi, kwa kweli mnafanya kazi kubwa na nzuri,” alisema.
Ameongeza, “Tunao vijana wengi ambao wana ndoto ya kuwa madaktari bingwa kama ambavyo Maria ametueleza ndoto yake, vijana wa chipukizi, tunaomba JKCI muwalee ili waweze kufikia ndoto zao hizo, kwani hii ni hazina ya Taifa letu.
Akizungumza, Maria amesema alidhamiria kusoma udaktari na kubobea katika masuala ya moyo tangu alipokuwa akisoma mkoani Mbeya.
“Tulipofanya ziara za kimasomo katika hospitali mbalimbali, nilikuwa nashuhudia jinsi ambavyo watanzania wenzangu wakubwa kwa wadogo wanavyoteseka kwa kuugua magonjwa haya.
“Nikaweka bidii katika masomo yangu, namshukuru Mwenyezi Mungu amenisaidia nimefanya vizuri, nawashukuru wazazi wangu kwa kuniwezesha kila hatua, walimu wangu kwa kunifundisha kwa moyo na wanafunzi wenzangu kwa ushirikiano wao,” amesema.
Baba mlezi wa Maria, Leonard Manyama amesema matokeo ya binti huyo yaliwashangaza. “Alianza kutueleza juu ya ndoto yake ya kuwa daktari kabla hata hajafanya mtihani, alianza kutafuta shule ya kwenda kusoma kwenye mtandao, akasema Feza Sekondari itamfaa, tukaendelea kumfuatilia kwa ukaribu, matokeo yake yalipotoka tulistaajabu, amefaulu kwa kiwango cha juu na Feza wamekubali kumsomesha bure,” amesema.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Tiba Shirikishi ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa JKCI, Delila Kimambo amempongeza msichana huyo kwa kuamua kutembelea taasisi hiyo kujifunza.
“Nimekubali kuwa mlezi wake, nitamsaidia popote pale atakapokuwa akihitaji msaada ili aweze kufikia ndoto yake,” alisema Dk. Kimambo.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...