WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema zaidi ya sh. bilioni 500 zimelipwa kwa
wakulima wa korosho kati ya sh. bilioni 700 zinazotarajiwa na kwamba
malipo hayo bado yanaendelea kulipwa kwa wakulima wengine waliosalia.
Amesema
tamko la Rais Dkt. John Magufuli la kwamba Serikali itanunua korosho
kwa bei ya sh. 3,300 ni kwa ajili ya korosho za daraja la kwanza na bei
ya korosho za daraja la pili ni asilimia 80 ya zile za daraja la
kwanza.
Ametoa
kauli hiyo leo asubuhi (Alhamisi, Februari 7, 2019) Bungeni jijini
Dodoma katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu
wakati akijibu swali la Mbunge wa Liwale, Zuberi Kuchauka.
Mbunge
huyo alitaka kupata kauli ya Serikali kuhusu malipo kwa wakulima wa
korosho ambao walikuwa wakilipwa sh. 2,600 kwa kilo wakati Rais
Dkt. Magufuli alisema Serikali itanunua kilo moja ya korosho kwa sh.
3,300.
“Malipo
yanaendelea na sehemu kubwa ni kwa wakulima wenye kilo zaidi ya 1,500,
Serikali itanunua korosho zote kama ilivyoelezwa. Taratibu zinazofanyika
ni kuhakikisha anayelipwa ni muhusika. Wananchi endeleeni kuiamini
Serikali yenu.”
Waziri
Mkuu amesema ilikuwa ni lazima kwa Serikali ifanye uhakiki kwa wakulima
hususani wale wenye kilo zaidi ya 1,500 ili kujiridhisha kama ni
wakulima, hivyo baada ya kuhakikiwa wakulima wote watalipwa fedha zao.
Amesema Januari 27, 2019 alitoa maagizo kwa
Wizara ya Kilimo pamoja na Bodi ya Mazao Mchanganyiko wahakikishe hadi
Februari 15 mwaka huu wawe wamekamilisha zoezi la uhakiki na kuwalipa
wakulima wote wa zao la korosho.
Waziri
Mkuu alitoa agizo hilo wakati akizungumza na wadau wa zao la korosho
kwenye kikao kilichofanyika mkoani Mtwara, lengo la kikao hicho ilikuwa
ni kupata taarifa juu ya mwenendo mzima wa bidhaa hiyo kwa msimu wa
mwaka 2018/2019.
Wakati huo huo,
Waziri Mkuu amesema Serikali haijakiuka sheria kuhusu suala la
watumishi kupandishwa mishahara na kwamba ina nia njema ya kuhakikisha
wanalipwa mishahara na posho nzuri.
Ameyasema
hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Mbozi, Pascal Haonga aliyedai
Serikali imekiuka sheria ya utumishi kwa kutopandisha mishahara, ambapo
Waziri Mkuu amesema Serikali haikukiuka sheria, bali iliamua
kushughulikia suala hilo kwa kuanza na uhakiki wa watumishi.
Waziri
Mkuu amesema baada ya kufanya uhakiki na kubaini uwepo kwa watumishi
hewa pamoja na waliokuwa wakitumia vyeti vya kugushi, iliwaondoa na sasa
Bodi ya Mishahara na Maslahi ya Watumishi wa Umma inafanya mapitio ya
mishahara baada ya kubaini tofauti, hivyo watumishi waendelee kuwa
watulivu.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
41193 - DODOMA.
ALHAMISI, FEBRUARI 7, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisikiliza swali kutoka Mbunge wa Mchinga, Hamidu Hassan Bobali ambaye aliuliza swali katika kipindi cha Maswali kwa Waziri Mkuu, Bungeni jijini Dodoma, Februari 7, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijibu maswali, Bungeni jijini Dodoma, Februari 7, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipongezwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji , Angela Kairuki baada ya kujibu vizuri sana maswali ya papo kwa papo, Bungeni jijini Dodoma, Februari 7, 2019. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...