Na Moshy Kiyungi,Dar es Salaam
Msanii mkongwe Afrika Kusini Yvonne Chakachaka akishirikiana na msanii wa nchini Tanzania Ali Kiba, waliachia rasmi wimbo wao mpya unaoitwa ‘Akili ya Mama’.
 Wimbo huo waliurekodi mwishoni mwa mwaka 2016 jijini Johannesburg, nchini Afrika ya Kusini, ambako Kiba alikuwa ameenda kutumbuiza kwenye tuzo za Mkhaya Migrants Awards.
Akiongea  jijini Dar es Salaam, mapema mwezi huu wa Mei, 2018, Chakachaka alisema wimbo huo ambao amefanya na Ali Kiba,  unawatetea akina mama.
 “Mimi na Ali tumeandika wimbo pamoja, una vibe ya “Mkomboti na tumeimba kwa lugha ya Kiswahili, Ali yupo Comfortable sana kuimba kwenye Kiswahili na amenifundisha kiasi kidogo cha Kiswahili” alisema Chakachaka.
Yvonne aliongeza akisema kuwa “Wimbo huo unawatukuza akina Mama,  Ali anaonekana ni kijana mzuri sana na namshukuru sana kwa kuimba wimbo wa kunitukuza mimi kama Mama na wanawake wengine Afrika.”
Msanii huyo mkongwe wa muziki kutoka Afrika Kusini, amemmwagia sifa lukuki mtunzi na mwimbaji Ali Kiba ‘Mvumo wa Radi’ kwa madai kuwa ni msanii mwenye kipaji cha hali ya juu.
Chakachaka alikuwepo nchini Tanzania kwa ajili ya shughuli za kijamii.
 Yvonne Chaka Chaka ni nani?

Wasifu wa Yvonne Chaka Chaka unaeleza kuwa alizaliwa mwaka 1965 nchini Afrika ya Kusini, akapewa majina ya Yvonne Machaka.
Ni msanii anaye heshimika zaidi nchini humo,  kwa akijihusisha na masuala ya misaada ya kibinadamu na ualimu.Chaka Chaka alipewa jina la ‘Princess of Africa’ kwa mafanikio makubwa kimuziki aliyoyapata kwa miaka 27.
Nyimbo zake zilizotamba ni pamoja na I’m Burning Up, Thank You Mister DJ, I Cry for Freedom, Makoti, Motherland na Umqombothi ambao ulitumika kwenye filamu ya mwaka 2004, Hotel Rwanda.Sifa za Yvonne katika muziki zilivuma zaidi mnamo miaka ya 1980. Kwa juhudi zake, hivi sasa ni mtangazaji na mwendesha kipindi katika kituo cha New Millennium.

Vilevile Chakachaka ni mburudishaji maarufu wa Afrika Kusini na Afrika kwa ujumla.Kwa mara ya kwanza alitikisa katika muziki wa Afrika Kusini, akiwa kijana mnamo mwaka 1984 kwa wimbo wa “I’m in Love with a DJ”.

Muziki wa disko uliotengenezwa na Sello ‘Chicco’ Twala ambao ulikuwa kama muziki wa asili ya Mbaganga, lakini ukiwa na mashairi ya Kiingereza.
 Mtindo huo Mbaganga uliweza kujulikana kama ‘Bubblegum’.
Yvonne Chakachaka sambamba na Brenda Fassi, walibaki wakitamba kwa miaka hiyo ya 1980.

Licha ya kuwa na umri mkubwa, haiba yake yenye mvuto wa pekee bado ipo vilevile.Aidha sauti yake nyororo ilijidhihirisha katika albamu ya Umqombothi mwaka 1988, ambayo ilipendwa na watu wengi.

Albamu hiyo ambayo ilikuwa inasifia pombe ya Kiafrika inayotokana na mtama ilikuwa katika mtindo wa Pop. Ingawa ilifuata kwa karibu desturi za Mbaganga na Singalong katika kiitikio, ambapo iliweza kuwavutia watu wa Afrika Kusini na Afrika kwa ujumla.

Aidha kulikuwa wimbo uliokuwa na jina lilelile la “I’m Love with a DJ”.


Alifanya ziara katika Afrika kwa kufanya matamasha katika viwanja vya Nigeria, Kenya na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (zamani Zaire).

Chaka chaka mekuwa msanii wa muziki wa Afrika nzima na anaendelea kufurahia hadi leo.Alitambulika kama “Malkia wa Afrika” kutokana na kutembelea Bara la Afrika na uvaaji wake wa kilemba kichwani.

Kwenye miaka ya 1990, Yvonne  aliendelea kufanya ziara na kuuza albamu katika kila nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara.Ikumbukwe kuwa aliwahi kutumbuiza katika kundi la viongozi  wa nchi za Afrika pamoja na tukio la kihistoria la kuzaliwa kwa nchi ya Afrika Kusini. 

Mwanamama huyo pia ni mlezi wa mradi wa ‘Giving and Sharing’ ambao unajishughulisha na kusaidia maskini wenye uhitaji, pia inajihusisha ukusanyaji wa mapato ili kupambana na gonjwa la Ukimwi,mfano ni kituo cha Orlando Children’s Home.
  
Aliachia albamu ya ‘Yvonne and Friends’ mwishoni mwa mwaka 2000, ambayo iliwashirikisha wasanii wa kigeni kama vile Tsepo Tshola ambaye alikuwa Sankomota.

Mwaka 2002 alifanya kazi ya kuwa mtangazaji katika radio na Televisheni, hii ilipelekea yeye kuhama kutoka kuwa ‘Malkia wa Afrika’ mpaka kuwa mfanyabiashara maarufu, mburudishaji na muelimishaji.

Yvonne Chaka chaka ameolewa na mwanafizikia kutoka Soweto na ni mama wa watoto wanne.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...