Na Shani Amanzi,
Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Simon Odunga amewaasa wananchi wa Chemba
kuacha tabia ya kupuuza wito wa Viongozi wa Serikali na taarifa mbalimbali zinazowahamasisha juu
ya maendeleo kwani zoezi la usajili na
utoaji wa vyeti vya kuzaliwa ni kwa manufaa ya kwao.
Odunga aliyazungumza hayo alipokuwa akizindua zoezi la
usajili na utoaji wa vyeti vya kuzaliwa
vya watoto waliochini ya miaka mitano(5) chini ya Rita kwa kushirikiana na
UNICEF pamoja na TIGO lililofanyika
tarehe 19/3/2019 katika viwanja vya Godown.
Odunga alisema "Ifikie mahali suala la hiari litoke na iwe lazima kwani vyeti vya
kuzaliwa kwa watoto ni muhimu sana katika maisha yao ya kila siku,kwani vyeti
vya kuzaliwa vinatumika kwenye uandikishaji kuanzia darasa la kwanza na Chuo Kikuu kwenye kuchukua mikopo kwa
wanafunzi,tumieni fursa hiyo kwa kuwa
awamu ya kwanza ni bure"
Ningependa zoezi hili Watendaji na Wenyeviti waweze kushirikiana nao
bega kwa bega katika kutoa taarifa hasa
kwa wale ambao hawajaandikisha watoto wao na kwa wale wanaogoma hatua kali
zichukuliwe,pia nawapongeza wakinamama kwa kuweza kuitika wito wa kuwaandikisha
watoto wenu kupata vyeti lakini kumbukeni kasi inahitajika zaidi .
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Dkt.Semistatus H.Mashimba amesema katika zoezi hilo lilianza na semina
kwa Watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Chemba iliyofanyika tarehe 7/3/2019
mpaka tarehe 9/3/2019 na Wahudumu wa afya na watendaji walipata semina hiyo
kuanzia tarehe 11/3/2019 hadi 13/3/2019
Aidha zoezi la usajili na utoaji wa vyeti lilianza rasmi tarehe
15/3/2019 na kuisha tarehe 28/3/2019 na
mpaka leo watoto waliosajiliwa taarifa zao kuingizwa kwenye mfumo wa taarifa
kwa njia ya simu .
Vilevile Mratibu wa zoezi hilo kwa wilaya ya Chemba Afisa Ustawi wa
Jamii wa Wilaya Bi.Euphrezia Anthony amesema zoezi linaenda vizuri pamoja ya
kuwa changamoto hazikosekani.
Ameeleza
kuwa Changamoto wanazokumbana nazo
kwenye zoezi hilo ni pamoja na baadhi ya kata kukosekana kwa mtandao,upungufu
wa magari 2pamoja na ugeni wa simu za kisasa kwa watendaji na wahudumu wa afya
lakini wanajitahidi kuzikabili kwa kuongeza timu ya usajili kwa njia ya simu na
kuongeza gari la pili ili kuhakikisha wanakamilisha zoezi hilo.

Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Simon Odunga akikabidhi cheti kwa mmoja wa akina mama aliyeshiriki hafla ya uzinduzi wa usajili na utoaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto waliochini ya miaka mitano (5) chini ya Rita kwa kushirikiana na UNICEF pamoja na TIGO lililofanyika Machi 19,2019 katika viwanja vya Godown wilayani humo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Dkt.Semistatus Mashimba akifafanua jambo kabla ya uzinduzi wa tukio hilo kufanyika .

Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Simon Odunga akizungumza mbele ya baadhi ya Wananchi alipokuwa akizindua zoezi la usajili na utoaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto waliochini ya miaka mitano (5) chini ya Rita kwa kushirikiana na UNICEF pamoja na TIGO lililofanyika Machi 19,2019 katika viwanja vya Godown wilayani humo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...