DEREVA, Geofrey Elifuraha mkazi wa jijini Dar es Salaam,  amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni akikabiliwa na  tuhuma za kuendesha gari kizembe. 

Katika kesi hiyo namba 257/2019 mshtakiwa huyo amesomewa Shtaka lake hilo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Hanifa Mwingira. 

Imedaiwa Kuwa, February 5 mwaka huko Kinondoni Hananasifu Mtaa wa Mkulima,  uliopo Katika Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam mshtakiwa Elifuraha alitenda kosa hilo. 

Imedaiwa, siku ya tukio,  mshtakiwa akiwa dereva anayeendesha gari namba T. 859CYT aina ya Toyota Noah, aliendesha gari hilo kwa uzembe na kushindwa kulimudu, hatimae akatoka nje ya barabara kisha kugonga mti na kusababisha uharibifu wa gari hilo.

Hata hivyo mshtakiwa huyo amekiri kutenda kosa hilo na amehukumiwa kulipa faini ya Sh. 30,000 ama kutumikia kifungo cha  miezi sita gerezani.

Aidha Mahakama imechukua leseni ya dereva huyo kwa kipindi cha mwezi mmoja. Hata hivyo dereva Elifuraha alifanikiwa kulipa faini hiyo na kufanikiwa kukwepa kifungo hicho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...