Leandra Gabriel, Globu ya jamii
SUMIKO Iwamura mwanamke(83) kutoka nchini Japan ndiye Dj wa klabu mzee zaidi duniani aliyetambulika na Guiness World Record ambaye hadi sasa anafanya shughuli hiyo.

Sumiko Iwamura maarufu kama Dj Sumirock alizaliwa Januari 23, 1934 na alikuwa na ndoto za kuwa mtu maarufu duniani kote lakini baada ya baba yake kufungua mgahawa alienda kusaidia hapo mara baada ya kumaliza shule.

Dj Sumirock alienda shule na kujifunza fani hiyo akiwa na miaka 77 na kuanza kufanya kazi hiyo mara mbili kwa mwezi huku akiendelea na kazi ya kuuza mgahawa.

Akiwa na ndoto za kusafiri duniani kote Dj Sumirock amesafiri katika nchi mbalimbali zikiwemo Paris na Newzealand huku akieleza kupendezwa za muziki wa Jazz na Rock.

Alipoulizwa na jarida la Guiness World Report kuhusiana na fani hiyo alieleza kuwa, "Ninafikiri  nilizaliwa na kipaji hiki na huwa sifanyi mazoezi kwa ajili ya afya ila ninapopiga muziki naona nafanya kitu cha  tofauti, nahisi nna nguvu" ameeleza Dj. Sumirock.

Kuhusiana na vijana wanaopambana kutimiza ndoto zao  Dj. Sumirock alinukuliwa akisema kuwa, "Nafasi  zipo kila siku, wasikate tamaa na daima wasisite kujaribu kitu" alieleza.

Dj. Sumirock ana ndoto za kusafiri duniani kote kwa kazi yake ya kupiga muziki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...