Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

CHINA ni moja ya nchi ambayo imekua mstari wa mbele  katika kukuza uchumi wake ikiwa ni pamoja na kujenga mazingira ya kuvutia na tofauti zaidi duniani, vitu vingi vya kustaajabisha na kushangaza vimekuwa vikitokea nchini humo na hiyo ni kutokana na kukua kwa teknolojia nchini.

Mtandao wa Chinawhispers wa nchi humo umetoa orodha ya vijiji kumi ambavyo ni tajiri zaidi nchini humo.

1. Kijiji cha Daqiuzhuang
Kijiji hiki kinapatikana katika Mji wa Tianjin na imeelezwa kuwa awali kilikuwa kijiji tajiri zaidi nchini humo, na ilipofika mwaka 1976 mwenyekiti wa kijiji hicho Yu Zuomin aliongoza wakulima katika ujenzi wa viwanda hapo ndipo kijiji hicho kilipoanza kupata utajiri lakini mwaka 1993 kiongozi huyo Yu Zuomin alikamatwa na kufungwa jela hapo ndipo uchumi wa kijiji hicho ukaporomoka. Uchumi wa kijiji hicho umefikia dola za kimarekani 180.

2. Kijiji cha Huaxi
Kijiji hiki kinapatikana katika Mji wa Jiangsu na kinafahamika zaidi kama "kijiji namba moja chini ya anga" na imewahi kuelezwa kuwa ndicho kijiji tajiri zaidi nchini humo, kilianzishwa mwaka 1961 huku ikielezwa wenyeji wa kijiji hicho  wana utajiri wa yuan 1500  na zaidi.Kijiji hicho kina sekta mbalimbali ikiwemo viwanda pamoja na makampuni ya kubadilisha fedha na tayari wamenunua ndege na kupanga kununua meli yao binafsi pamoja na kufungua hoteli ya kimataifa  ambayo ilifunguliwa wakati kijiji hicho kikisherekea miaka 50 tangu kuanzishwa kwake.

3. Kijiji cha Liuzhuang
Kinapatikana katika eneo la Henan na kilijulikana kwa kuwa kijiji maskini zaidi miaka iliyopita, kwa sasa kinamiliki zaidi ya dola milioni 120  na kina utajiri zaidi  katika sekta za makazi, shule nzuri, pamoja na huduma za afya ambazo hutolewa bure na kila familia kijijini humo kinamiliki takriban dola 24,000.

4. Kijiji cha Nanling
Hiki kinafahamika kama kijiji cha kwanza nchini China na viongozi wakubwa nchini humo Jiang Zemin na Hu Jintao waliwahi kutembelea kijiji hicho mwaka 2008, huku mali zao zikifikia Yuan 1.3 bilioni na mapato kwa wanakijiji yakifikia Yuan 150,000.

5. Kijiji Tengtou
Ni kijiji tajiri zaidi katika eneo la Zhejiang na hadi sasa zaidi ya watu 800 wanaishi kijijini hapo, na hadi kufikia mwaka 2009 uchumi wake ulikua hadi kufikia Yuan 5.5 bilioni.

6.Kijiji cha Nanjie
Kinapatika katika eneo la Henan kikiwa na makazi zaidi ya 3100 na idadi kubwa ya wakomunisti pamoja na huduma zinazotolewa bure zikiwemo elimu, afya,makazi, chakula pamoja na mishahara kwa wafanyakazi wa viwanda wanaolipwa dola 400.

7. Kijiji cha Huayuan
Kinapatikana katika Mji wa Jinhua huko Zhejiang, ni kijiji maarufu nchini humo, mapato ya wanakijiji ni Yuan 16,520 na mwaka 2005 kijiji kilitengeneza mapato ya  zaidi ya Yuan bilioni 1.729.

8. Kijiji cha Dazhai
Ni kijiji maarufu zaidi kikiwa na vivutio vya kutosha pamoja na kupata zaidi ya watalii 200,00 kwa mwaka huku mapato ya mwaka 2005 yakifika jumla ya Yuan milioni 116  huku mapato ya mwaka yakifikia Yuan milioni 5500.

9. Kijiji cha Shenquanzhuang
Kinapatikana karibu na eneo la Shandong likiwa na wanakijiji 1600 mwaka 2002 likiwa na mapato ya zaidi ya Yuan bilioni 2.69 kwa mwaka.

10.Kijiji cha Hangmin
Kinapatikana karibu na Zhejiang na kijiji tajiri zaidi Zheijiang, huku ikielezwa mapato ya wanakijiji  ni Yuan 35,000 na wanakijiji wakiwa na maisha bora zaidi.

Nini Maoni yako kuhusu vijiji bora na tajiri zaidi nchini?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...