Awa Rais Mkongwe zaidi anayeishi nchini Marekani, Avunja rekodi ya Rais George H.W Bush aliyefariki akiwa na miaka 94 na siku 171

Na Leandra Gabriel, Blogu yajamii
ALIYEKUWA Rais wa 39 wa  Marekani Jimmy Carter amevunja rekodi kwa kuwa Rais mzee zaidi anayeishi nchini humo.

Amepewa cheo hicho leo Machi 22 mara baada ya kufikisha miaka 94 na siku 172 akivunja rekodi iliyokuwa inashikiliwa na aliyekuwa Rais wa awamu ya  41 George H.W Bush ambaye alifariki  mwezi Novemba mwaka jana akiwa na umri wa miaka 94 na siku 171.

Catter alizaliwa October 1, 1924 na alihudumu kama Rais wa 39 wa Marekani kuanzia 1977 hadi 1981 na kabla ya kuhudumu nafasi hiyo amewahi kushika nyadhifa katika ngazi za Bunge kwa miaka ipatayo 10.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...