Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
MACHO
yangu yanashuhudia kazi kubwa na nzuri inayofanywa na Shirika la Umeme
Tanzania(TANESCO) chini ya Wizara ya Nishati kwa niaba ya Serikali ya
Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dk.John Magufuli.
Kubwa zaidi
masikio yangu kwa miaka miwili sasa yamekuwa yakisikia sifa zikitolewa
kwa TANESCO kwasababu tu yale mambo ya kukatika katika kwa umeme
yamepungua .Tulizoea kuita mgao.Mara umeme unatika...mara huooooo
umerudi.Leo hii umeme ukikatika basi ni kwasababu maalumu na umma
utakuwa umeshapata taarifa mapema.Mbona raha jamani.
Kwangu mimi
najaribu kuiangalia TANESCO ya sasa na ile ya zamani.Kuna tofauti kubwa
ya kiutendaji.TANESCO ya sasa chini ya Mkurugenzi Mtendaji wake Dk. Tito
Mwinuka inajua umuhimu wa nishati ya umeme.Inajua kabisa uchumi wetu
unahitaji uwepo wa umeme wa uhakika katika kufanya shughuli zao za kila
siku.
TANESCO inayoongozwa na Dk.Mwinuka inajua umuhimu wa kutoa
taarifa kwa wananchi hasa pale ambapo kutakuwa na matenengezo katika
eneo fulani.TANESCO ya sasa inajua kuwa Serikali ya Awamu ya Tano
inataka kuelekea uchumi wa kati ambao utachagwiza na umeme wa uhakika.
Pia
inatambua fika kama kuna eneo ambalo lilikuwa linalalamikiwa ni
kukatika kwa umeme.Mgao wa umeme ulikuwa kero kwa watu wengi.Tena kero
haswaa na najua sio kwangu tu hata kwako.Ndio mgao ilikuwa
kero.Unabisha?
Serikali ya Awamu ya Tano kwa kutambua nchi yoyote
ili iendelee inahitahaji kuwa na nishati ya umeme wa kutosha na
uhakika.Ndio maana leo hii TANESCO inaendelea na ujenzi wa miradi
mikubwa na midogo ya umeme ambayo ipo katika hatua mbalimbali za
utekelezaji wake.
Kutekelezwa kwa miradi hiyo na hasa kwenye
maeneo ambayo awali yalikuwa na tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa
mara leo hii hakuna tena mgao.Wananchi wanafurahia nishati hiyo ya umeme
wa uhakika.Ukitaka kuamini hili inaloeleza hapa nenda mikoa ya
Kaskazini ikiwemo ya Arusha na Kilimanjaro.Hawana tena tatizo la
kukatika kwa umeme kama zamani.
Sote tunafahamu kabla ya Awamu ya
Tano kuingia madarakani kulikuwa na changamoto kubwa ya umeme.Leo hii
imebaki historia.Umeme unaozalishwa Mkoa wa Arusha umekidhi mahitaji na
kufanya kuwepo na umeme wa akiba.Hivyo ninaposema TANESCO inastahili
pongezi sio kwamba natoa sifa sehemu ambayo haistahili.
Hongereni
TANESCO kazi ambayo mnaifanya kwa niaba ya Serikali ya Awamu ya Tano ni
kubwa na tunaiona. Pamoja na mambo mengine , TANESCO kwa sasa
wanaendelea na majukumu ya kuendelea kutatua changamoto zilizopo kwenye
sekta ya nishati ya umeme.
Na si tu kuondoa changamoto,pia
imeendelea na wajibu wake mkubwa kusambaza umeme kwa wananchi.Nafahamu
jitihada za kupeleka umeme kwa kila kijiji ndani ya nchi yetu kupitia
Wakala wa Umeme Vijijini (REA).
Naomba niwe mkweli na msema kweli
ni mpenzi wa Mungu.Hakika Wizara ya Nishati na TANECSO wanafanya kazi
kubwa ya kuhakikisha umeme unafika kwa kila Mtanzania anayeuhitaji.Kwa
siku mbili hizi nimekuwa nikishuhudia baadhi ya nyumba tena za matembe
zikiwa zimewekwa umeme.
Kwa muda mrefu tumekuwa tukisikia tu,
umeme unawekwa vijijini ila kwa bahati mbaya tupo baadhi yetu ni kama
Tomaso.Bila kuona hakuna kuamini.Sasa tunaamini kumbe kweli.Hivyo uwepo
wa picha hizo ambazo zinaonesha nyumba za udongo zikiwa zimewekwa umeme
inaleta maana halisi ya kile ambacho Wizara ya Nishati inafanya kwa
wananchi wake.
Tunafahamu kauli mbiu ya TANESCO imekuwa ikisema
"Tunaangaza maisha" .Nimeamini hata uwe kijijini bado utaangaziwa
maisha.Hili ni jambo jema na la kupongezwa.Umeme wa uhakika vijijini ni
jambo la msingi sana, na tunafahamu kwa muda mrefu vijiji vyetu vilikosa
maendeleo kwasababu ya kutokuwa na umeme.Leo wanao.
Kwa
waliobahatika kuishi maeneo ya vijijini wanafahamu mazingira ya kutokuwa
na umeme.Wana vijiji wanalazimika kutembea umbali mrefu kutafuta
nishati ya umeme.Ameaniaka mahindi au mpunga wake lakini linapofika
suala la kusaga au kukoboa anawaza umbali wa kwenda mashineni.Leo hii
hakutakuwa na kuwaza tena.
Umeme unapatikana kila mahali.Shida
iko wapi? Hata hivyo, kuna baadhi ya watu kwenye mitandao nimeona
wakijadiliana na wengine kuhoji kwanini umeme unawekwa kwenye nyumba za
tembe ambazo kuta zake zinatengenishwa na udongo.Kwangu naona wanaohiji
hayo ni kama vile wamekosa hoja.
Watalaam wamejiridhisha na
wanajua hakuna madhara yoyote kwani kuna vifaa maalum vinavyotumika
katika kuunganisha umeme kwenye nyumba hizo.Nitoe rai kwa Wizara ya
Nishati pamoja na TANESCO endeleeni na majukumu yenu ya kuweka umeme
vijijini.Kwa maisha ya sasa nishati ya umeme ambayo ni ya uhakika
inahitajika sana kuliko nyakati nyingine zozote.Huo ndio ukweli.
Kwanini
bibi na baba yangu waendelee kuteseka? Eti washindwe kuwa na luninga
pale sebuluni kisa tu wapo kijijini.Eti waendelee tu kutumia vibatari
.Hapana bwana lazima ifike mwisho.Walioko vijijini ni Watanzania na wana
haki ya kupata umeme kama wengine wanaoishi maeneo ya mijini.
Tunafahamu
kuna baadhi ya familia ambazo ziko mjini na zilishindwa kutembelea
ndugu , jamaa na marafiki walioko vijijini na sababu tu ni kwamba eti
wakienda huko hakuna umeme na wanasema hawawezi kutumia vibari.Kufungwa
kwa umeme katika nyumba zetu za vijijini ambako wengi ndiko tunatokea,
kunakwenda kufanya mabadiliko makubwa.
Mjini umeme upo na kijiji
nako upo.Ukiishi kwenye ghorofa utakuwa na umeme na ukiishi kwenye
nyumba ya tembe utakuwa na umeme.Hongereni TANESCO. Kufungwa umeme
kwenye nyumba za vijijini kunakwenda kuifanya Tanzania kuwa yenye
maendeleo.Kokote Mtanzania alipo na anahitaji umeme kwa ajili ya ujenzi
wa maendeleo ya nchi yetu.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ameizindua nyumba ya Rose Kagoma iliyounganishiwa umeme wa REA katika Kijiji cha Ruganga Wilayani Kibondo.Katika hafla hiyo iliyofanyika Machi 24 mwaka huu, Waziri Kalemani amewataka Wandarasi kutokubagua Wananchi kwenye mradi huoKijiji cha Rugunga kimeunganishiwa umeme kupitia mradi wa umeme Vijijini wamu ya tatu sehemu ya kwanza(REA)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...