Taarifa hii inatoa muhtasari wa mwelekeo wa hali ya hewa wa muda mfupi na muda
wa kati kwa lengo la kuwapatia wananchi taarifa sahihi na za ziada kuhusu utabiri wa
mvua iliokwishatolewa.
Mwenendo wa mvua katika kipindi hicho hautarajiwi kubadili matarajio ya jumla ya
mvua za Masika. Hivyo, msimu unatarajiwa kuwa mfupi na vipindi vya upungufu wa
mvua za Masika vikijitokeza katika maeneo mengi.
Mvua zinatarajiwa kunyesha katika maeneo mengi yanayopata mvua za Masika baada
ya athari ya upungufu wa mvua uliotokana na vimbunga vilivyojitokeza mfululizo
katika bahari ya Hindi ikiwemo kimbunga Idai, Savannah na Joaninha katika mifumo
ya hali ya hewa kuanza kupungua. Vipindi vya mvua vinatarajiwa kuongezeka katika
baadhi ya maeneo katika wiki mbili zijazo za mwezi Aprili, 2019.
Aidha, maeneo ya mikoa ya Dodoma, Singida, Manyara na Kilimanjaro ambayo
yalikumbwa na upungufu wa mvua kutokana na vimbunga hivyo, yanatarajiwa
kuanza kupata mvua katika kipindi hiki cha mwishoni mwa mwezi Machi na wiki ya
kwanza ya mwezi Aprili, 2019. Ongezeko la mvua linatarajiwa katika baadhi ya
maeneo ya mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara hususan katika wiki ya pili ya
mwezi Aprili, 2019 kwa siku chache.
ANGALIZO
Vipindi vya mvua kubwa vinatarajiwa kujitokeza katika maeneo yafuatayo katika muda uliotajwa.
Vipindi vya mvua kubwa vinatarajiwa kujitokeza katika maeneo yafuatayo katika muda uliotajwa.
i. Vipindi vifupi vya mvua kubwa vinatarajiwa katika baadhi ya maeneo ya
nyanda za juu kusini magharibi (mikoa ya Iringa, Njombe, Mbeya,
Songwe, Rukwa na Morogoro-Mahenge) na mikoa ya Lindi na Mtwara
katika kipindi cha mwisho wa wiki kuanzia tarehe 30 Machi hadi 3 Aprili,
2019.
ii. Mwanzoni mwa mwezi Aprili, 2019 vipindi vifupi vya mvua kubwa
vinatarajiwa kujitokeza katika mkoa wa Morogoro na kusambaa katika
maeneo machache ya mikoa ya Pwani na Dar es Salaam.
HALI YA JOTO
Wimbi la joto lililojitokeza katika kipindi cha upungufu wa mvua katika maeneo ya pwani ya kaskazini na nyanda za juu kaskazini mashariki linatarajiwa kupungua kiasi katika kipindi cha uwepo wa mvua.
Wimbi la joto lililojitokeza katika kipindi cha upungufu wa mvua katika maeneo ya pwani ya kaskazini na nyanda za juu kaskazini mashariki linatarajiwa kupungua kiasi katika kipindi cha uwepo wa mvua.
USHAURI: Wananchi wanashauriwa kuendelea kufuatilia taarifa za utabiri kutoka
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania na kuzingatia tahadhari zilizotolewa na mirejeo
yake pamoja na kupata na kuzingatia ushauri na miongozo ya wataalam katika sekta
husika ili kupunguza athari zinazoweza kujitokeza.
Imetolewa tarehe 29 Machi 2019 na:
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...