Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii

AKIWA anatumikia kifungo cha miaka 15 gerezani alichokianza mwaka 2013  Hamza Bendelladj aliyepewa jina la "Mdukuaji anayetabasamu", anatumikia kifungo hicho  kwa makosa ya udukuzi katika benki 217 nchini Marekani na kuathiri zaidi ya kompyuta milioni 50 za watumiaji na kuweka rekodi ya kuwa mmoja kati ya wadukuaji 10 katika orodha ya mashirika ya upelelezi ya FBI na Interpol.

Hamza raia wa Algeria alizaliwa mwaka 1988 kwa sasa ana miaka 31 na   anazungumza lugha zaidi ya tano zikiwemo Kiingereza, kiarabu na kifaransa huku akiwa na Shahada ya sayansi na teknolojia ya komputa katika chuo kikuu cha Bab Ezzouar.

 Hamza amekuwa akifanya udukuzi na kutumia fedha hizo kwa kuwasaidia watu wenye matatizo , aliwahi kudukua mtandao rasmi wa serikali ya Israeli na kuhamisha zaidi ya dola milioni 280 za kuzigawa katika taasisi zisizo za kiserikali (NGO'S) nchini Palestina ili kuwasaidia wahitaji.

Alikamatwa Januari 8, 2013 mpakani mwa Malaysia na Misri na hakukataa kukamatwa kwake, alitabasamu kila alipopelekwa mbele ya vyombo vya habari na mkewe pamoja na binti yake walikuwa naye pamoja na kila hatua na hata alipoulizwa ni wapi alipopeleka fedha hizo alijibu amepeleka kusaidia Palentina na nchi za Afrika.

Yanayowavuta wengi kumuhusu ni pamoja na  kuwa na matukio mbalimbali ikiwemo ya kutengeneza maunzi laini(software) aina ya SpyEye na kuitumia katika kuiba fedha pamoja na  kuiuza kwa wadukuzi wengine hali iliyopelekea kuathirika kwa  watumiaji milioni 50 wa kompyuta baada ya nywila zao kudukuliwa.

Pia aliwahi kuwa mmoja wa wanachama cha wadukuzi cha Darkode.com pamoja na mdukuzi kutoka nchini Urusi Aleksandr Andereevich aliyehukumiwa jela miaka 8 na nusu jela.

Licha ya taarifa za kusambaa kuwa kijana huyo amenyongwa mamlaka husika ilikanusha taarifa hizo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...