Arusha, 12 Machi, 2019 

Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomu (IAEA) kanda ya Afrika Profesa Shaukat Abdulrazak anatarajia kuonana na viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Marchi 13. 

Mkurugenzi huyo ataambatana na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Profesa Lazaro Busagara ambao watapata nafasi ya kufanya mazungumzo na viongozi mbali mbali. 

Mkurugenzi huyo aliweza pia kuhudhuria ufunguzi wa mkutano wa kimataifa wa waratibu (NLOs) wa miradi ya Sayansi na Teknolojia ya Nyuklia unaowahusisha nchi wanachama 46 wa Shirika la Nguvu za Atomu Duniani uliofunguliwa March 11 na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. William Ole Nasha unaoendelea jijini Arusha. 

Shirika la Nguvu za Atom duniani IAEA linatoa ufadhili kwa serikali ya Tanzania katika miradi mbali mbali inayohusisha sekta za Afya, Kilimo, Maji, Mifugo, Rasilimaliwatu, Nishati na Viwanda ambapo mpaka sasa ni jumla ya shilingi za kitanzania bilioni 9.5 zimetolewa kwa ajili ya ununuzi wa vifaa na gharama za mafunzo kwa wataalamu katika masuala ya afya. 

Imetolewa na; 
Kitengo cha Mawasiliano 
Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...