Habari na Picha na
Dixon Busagaga, Moshi
MVUA kubwa iliyoambatana na upepo imesababisha adha kwa watumiaji wa BARABARA kadhaa katika mji wa Moshi baada ya miti kukatika na kufunga barabara.
Globu ya Jamii imepita maeneo kadhaa ya mji wa Moshi na kujionea kadhia hiyo huku maeneo mengine wananchi wakijitolea kuondosha miti iloyoanguka barabarani kwa kuikata huku watumiaji wa vyombo vya moto wakilazimika kunadili njia za kupita .
Maeneo ambayo watumiaji wa vyombo vya moto wameathirika ni pamoja barabara ya Shanty town,barabara ya International school pamoja na barabara ya Shule ya sekondari Mawenzi.
Maeneo mengine imeshuhudiwa miundombinu ya umeme ikiwa imeharibika baada ya nguzo kukatika na nyaya kuangakua katikati ya barabara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...