Charles Ole Ngereza enzi za uhai wake
Mwenyekiti
wa Arusha Press Club (APC) Cloud Gwandu akiwa msibani nyumbani kwa
marehemu Charls Ngereza na baadhi ya waandishi kama wanavyoonekana
pichani.
Waandishi
wa habari wa vyombo mbalimbali Mkoani Arusha wakiwa msibani nyumbani
kwa Marehemu Charles Ngereza eneo linalofahamika kama Kwa Mrefu.
Na. Vero Ignatus, Arusha.
Mwandishi
wa habari aliyekuwa muwakilishi wa habari wa ITV na Radio one hatimae
idhaa ya Kiswahili DW mkoani na makamu mwenyekiti wa Arusha Press Club
Arusha Charles amefariki duania leo alfajiri
Marehemu
alianza kuugua mwishoni mwa mwezi December 2018 ambapo alianza
kupatiwa matibabu katika hospitali ya KCMC, ambapo alihamishiwa nchini
India kwa matibabu zaidi na baadae alirudi nyumbani na kuendelea
kujiuguza.
Hata
hivyo hali yake ilibadilika ghafla hapo jana mchana na kukimbizwa
katika hospitali ya Mkoa ya Mount Meru kisha kuhamishiwa Hospitali ya ST
Elizabeth Mkoani Arusha na kufariki dunia alifajiri ya leo
Kwa
upande wake mwenyekiti wa Arusha Press Club Cloud Gwandu amesema kuwa
msiba huo ni mzito kwa wanahabari wa mkoa wa Arusha kwani marehemu
alikuwa ni mchapakazi, asiyekuwa mvivu na alikuwa mtu wa viwango na
ubora.
Kwahiyo
kama kiongozi mwenzetu tumeshirikiana nae katika mambo mengi sana hata
hivi alipoondoka kuna mradi alituunganisha na wadau wake katika APC
wazaidi ya milioni 500 ambao utaleta manufaa kwa wanachama wa APC na
tunaamini kwamba wadau hao hawatausitisha
Waandishi
wahabari kwa pamoja Jijini Arusha wamesikitishwa kuondokewa mwenzao
hivyo ametoa pole kwa wanahabari na wote walioguswa na msiba huu.
Alisema Gwandu.
Nayo familia ya Marehemu ` na wanahabari Mkoani humu wanaendelea na maandalizi ya siku ya mazishi yatakayotangazwa baadaye.
Marehemu ameacha mke mmoja na watoto wawili mmoja wa kike na mwingine wa kiume.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina lake Lihimidiwe.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...