Bi.
Amina Jumanne Mkazi wa kipera ambaye ni kibarua katika ujenzi unaoendelea eneo
la Maekani akisalimiana na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (MB)
wakati alipotembelea shughuli ya Ujenzi inayoendelea.
Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (MB) akiwa na mwenyeji wake Makamu Mkuu wa Chuo sili Chuo Pro. Lughano Kusiluka; baada ya kuwasili Chuo Kikuu Mzumbe; alipofanya ziara hivi karibuni.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (MB) akiweka saini kwenye kitabu cha Wageni baada ya kuwasili Chuo Kikuu Mzumbe.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango akiwasili eneo la Maekani ambako ujenzi wa mabweni ya wanafunzi unaendelea. Kushoto ni Prof. Ernest Kihanga Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Utawala na Fedha, akifuatiwa na Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (MB), mwenye kofia ni injinia na msimimizi ya mradi Injinia Focus Alex Odecho, na wa mwisho kulia ni Prof. Lughano Kusiluka Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (MB) akielekeza jambo kwenye moja wapo ya majengo ya ujenzi wa hosteli za wanafunzi unaoendelea eneo la Maekani. Kulia ni msimamizi wa mradi Injinia Focus Alex Odecho.
Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (MB)
afurahia zawadi yenye kumbukumbu ya Chuo Kikuu Mzumbe alichosoma na kufanya
kazi kabla ya kuingia kwenye siasa.
Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (katikakati)
akiwa kwenye picha ya pamoja na Menejimenti ya Chuo Kikuu Mzumbe alipotembelea
hivi karibuni.
Naibu Waziri Fedha
na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (MB) ametembelea Chuo Kikuu Mzumbe na
kukagua ujenzi wa Mabweni ya Wanafunzi unaoendelea katika eneo la Maekani, Makao
Makuu ya Chuo hicho, Morogoro.
Mhe.
Naibu Waziri, amepongeza jitihada kubwa zilizofanywa na Uongozi wa Chuo kwa
kushirikiana na Serikali katika kutatua kero ya malazi kwa wanafunzi na
kusisitiza umuhimu wa kuanza mara moja awamu ya pili ya ujenzi wa vyumba vya
madarasa na mihadhara katika eneo hilo ili kuwarahisishia wanafunzi kutotembea
umbali mrefu wakati wa masomo.
“Serikali
inategemea mchango mkubwa wa Vyuo Vikuu katika kutimiza malengo; hasa kwenye
hili la ukuaji wa uchumi. Pamoja na kwamba tunajivunia uchumi wetu kukua lakini
tusibweteke, badala yake tufanye tafiti na kuandaa vema vijana ambao watakuwa
watumishi bora wa Umma wanaoendana na dhana ya sasa ya nidhamu ya kazi. Hivyo,
nimefarijika sana kuona maendeleo na hatua kubwa ambayo mmepiga kitaaluma na
katika miradi ya maendeleo mnayosimamia” alisema Mhe. Naibu Waziri.
Akikamkaribisha
Naibu Waziri huyo, ambaye pia alipata fursa ya kuzungumza na Menejimenti ya
Chuo Kikuu Mzumbe; Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Lughano Kusiluka amemweleza
Mheshimiwa Naibu Waziri kuwa, kwa sasa Chuo Kikuu Mzumbe kinatekeleza miradi
mbalimbali ya maendeleo ya miundombinu katika Kampasi Kuu ya Morogoro, Kampasi
ya Mbeya na Kampasi ya Dar-es-salaam na kwamba, lengo ni kuendelea kutumia
ruzuku inayotolewa na Serikali na vyanzo vya mapato ya ndani kuendeleza ujenzi
na kuboresha miundombinu ya Chuo ili kujenga mazingira bora ya utoaji wa Elimu
ya Juu.
“Napenda
kuipongeza sana Serikali yetu kwa kutambua mchango mkubwa wa Vyuo Vikuu nchini,
na kwa upande wa Taaluma, Chuo chetu kitaendelea kuunga mkono jitihada za
Serikali ya Awamu ya Tano katika kuendeleza Uchumi wa Viwanda; kwa kuendelea
kufanya tafiti, kubuni miradi ya maendeleo na kutoa nguvu kazi itakayowezesha
Tanzania kufikia malengo yake” alisema Prof. Kusiluka.
Ameahidi
Chuo Kikuu Mzumbe kuendelea kuimarisha uhusiano na kufanya kazi kwa karibu
zaidi na Taasisi na Mashirika mbalimbali ya Umma kwa kubadilishana ujuzi na
uzoefu, pamoja na kutumia wanataaluma kuboresha utendaji Serikalini, kulinda nidhamu
na kuinua kiwango cha elimu inayoendelea kutolewa na Chuo hicho.
Mradi
wa Ujenzi wa Mabweni katika Kampasi Kuu ya Chuo Kikuu Mzumbe ambao unafadhiliwa
na Serikali,unatekelezwa na SUMA JKT na unategemewa kukamilika ifikapo mwezi
Oktoba mwaka huu. Mradi unategemea kugharimu kiasi cha shilingi bilioni 6.5
hadi utakapokamilika. Kukamilika kwa mradi huu kutawezesha wanachuo wengi zaidi
katika Kampasi Kuu kukaa kwenye hosteli za Chuo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...