Mary
Sapali, Mratibu Wa Damu Salama Kanda ya Nyanda za Juu Kusini
akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Jiongeze Tuwavushe Salama
mkoani Njombe.
Dionisia
Simime, Mratibu Wa Damu Salama Halmashauri ya wilaya ya Njombe
akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Jiongeze Tuwavushe Salama
mkoani Njombe.
Dkt.Bumi Mwamasage, Mganga mkuu Wa mkoa Wa Njombe akizungumza wakati wa
uzinduzi wa kampeni ya Jiongeze Tuwavushe Salama mkoani Njombe.
Mhe. Christopher Ole Sendeka, Mkuu Wa mkoa wa Njombe, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Jiongeze Tuwavushe Salama.
Na. Vero Ignatus.
Kampeni
ya 'Jiongeze Tuwavushe Salama' imezinduliwa mkoani Njombe, ambapo Mkuu
wa Mkoa huo, Mhe. Christopher Ole Sendeka amewataka watendaji kufanya
kila wawezalo kuhakikisha kampeni hiyo inaleta tija kwa kupunguza vifo
vya mama wajawazito na watoto wachanga pindi wanapozaliwa.
Kuzinduliwa
kwa kampeni hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Serikali kwa
wakuu wote wa mikoa nchini katika kuhakikisha vifo vya wajawazito na
watoto wachanga vinapungua.
Kampeni
hiyo ilizinduliwa Kitaifa mwaka jana mkoani Dodoma na Makamu wa Rais
Mhe. Samia Suluhu Hassan, kuhudhuriwa na wakuu wote wa mikoa, akiwemo
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu.
Mhe.
Ole Sendeka amesema kampeni ya 'Jiongeze Tuwavushe Salama' ni ya
kitaifa, ikiwa chini ya Raisi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, hivyo
watendaji wajipange kuhakikisha malengo yanafikiwa.
"Naagiza
Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Njombe, Makatibu Tawala na Wakurugenzi
kuhakikisha hatua za kuzuia vifo, ikiwemo kutoa huduma za kitaalamu kwa
wakati na kuhakikisha vifaa tiba vinapatikana katika vituo vya Afya,"
alisema Ole Sendeka.
Amesema
serikali inafanya kila iwezalo kuhakikisha mama wajawazito wanapatiwa
ushauri, dawa, kuanzia kliniki hadi pale kujifungua salama
"Mhe Dkt. Magufuli, kwa kuwajali wananchi wake, ametupatia zaidi ya bilioni 3 ili tujenge vituo vya afya katika mkoa wetu, Wakuu
wa Wilaya katembelea maeneo ya ujenzi kila mara ili kuhakikisha ujenzi
sahihi, kwa matumizi sahihi ya fedha unafanyika," alisema Ole Sendeka.
Dkt.
Bumi Mwamasage ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Dkt. Bumi amesema
uwajibikaji wa kuhakikisha mama wajawazito wanajifungua salama unapaswa
kuanzia katika ngazi ya familia.
"Baba
na wana familia wanalazimika kuhakikisha mama anahudhuria kliniki ili
apate elimu ya ujauzito wake na umuhimu wa chanjo kwa ajili ya kujilinda
yeye na mtoto atakayemzaa.
Dkt.
Bumi amesema Kampeni hiyo ni ya mwaka mmoja katika mpango wa 'Life
Plan' wenye lengo la kuhakikisha hakuna tena vifo vya mama wajawazito na
watoto wachanga, hivyo inabidi jamii yote ishiriki elimu ya kutosha
itolewe katika kulikabili tatizo hilo.
Ofisi
ya Mkuu wa Mkoa iliahidi kuchangia shilingi 500,000 Mkuu wa Wilaya
100,000 kila Mkurugenzi, Wenyeviti wa halmashauri Waganga Wakuu
wakiahidi kutoa 50,000 ikiwa sehemu ya kuchangia upatikanaji wa Damu
Salama wakati wa mama anapojifungua na kutokwa damu nyingi ambao
miongoni mwao hupoteza maisha
Kampeni
ya Jiongeze Tuwavushe Salama inatekelezwa na Wizara ya Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na Mashirika yasiyo ya
kiserikali ikiwemo UNICEF.
Mwisho
Matukio mbalimbali wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Jiongeze Tuwavushe Salama mkoani Njombe.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...