Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 


Wakala wa Usalama na Afya Pahala Pa Kazi (OSHA)imesema kuwa nguvu kazi ya Taifa lazima ilindwe katika afya ili iweze kuzalisha kwa kujenga uchumi wa nchi.

Hayo ameyasema Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa OSHA Khadija Mwenda wakati wa mafunzo ya wafanyakazi wanawake wanaofanya usafi katika barabara za Manispaa ya Kinondoni na Ilala amesema kuwa wanawake ndio wazalishaji pamoja na wasimamizi wa familia hivyo serikali inaangalia katika jicho ya kulinda afya zao wasiweze kuteteleka na kushindwa kusimamia familia zao.

Amesema kuwa wanawake hao wanaweza kuwa wanafanya usafi lakini hawafahamu jinsi ya kulinda afya zao ambapo OSHA ndio kazi yao katika kuwajengea uwezo wa kutambua umuhimu wa afya zao katika sehemu za kazi zao.

Mwenda amesema kuwa katika kuelekea siku ya kilele cha maadhimisho ya siku wanawake duniani ambayo hufanyika Machi 8 ya kila mwaka OSHA imeona ni wakati mwafaka kutoa elimu ya wafanyakazi wanawake wa usafi katika baadhi ya barabara katika jiji la Dar es Salaam.

Aidha Mwenda amesema kuwa OSHA itaendelea kutoa elimu katika mahala pa kazi katika kuhakikisha uchumi wa viwanda unajengwa na nguvu kazi yanye afya imara." Tumedhamiria kutoa elimu pahala pa kazi katika kuimarisha Afya za wafanyakazi ya kutokuwa na madhara ya kazi kwa kuwa wana vifaa vya kuzuia madhara hayo"amesema Mwenda 

Amesema kauli mbiu ya OSHA katika siku ya wanawake ni 'Usalama wa Afya kwa kuzinagatia Usawa wa Kijinsia, Badiri Fikra Usawa wa Kijinsia kwa Maendeleo Endelevu.Katika mafunzo hayo OSHA imetoa vifaa kinga kwa wanawake hao ili waweza kutekeleza majukumu yao katika kujilinda na afya na usalama sehemu zao za kazi.

Nae Mfanyakazi wa Usafi Barabarani Halima Rajab amesema wanachangamoto kwa madereva ambao huwa wanawafaya kuwa waangalifu na bila kufanya hivyo wanagongwa.

Amesema wanaishukuru OSHA kwa kuwaandalia mafunzo kwani wanaamini serikali imewaona. Maendeleo ya Uchi kuhakikisha
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Pahala Pa Kazi (OSHA) Khadija Mwenda akizungumza wakati akifungua mafunzo ya wanawake wanafanya usafi katika barabara za jiji Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa usafi Barabarani wakiwa katika mafunzo ya OSHA
Baadhi ya wanawake na wamiliki wa kampuni za ukandarasi wa usafi wa barabara katika jiji la Dar es Salaam wakipatiwa mafunzo na OSHA.
Halima Rajab Mfanyakazi wa Usafi wa Barabara akizungumza na waandishi habari kuhusiana na changamoto wanazokutana katika usafi wa barabara wakati wa mafunzo ya OSHA ya wanawake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...