Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ametoa ahadi ya kuwasomesha kuanzia kidato cha tano hadi cha sita bure wasichana 100 waliofanya vizuri kwenye masomo ya sayansi katika matokeo ya mtihani wa kidato nne ili kuongeza idadi ya wanawake wataalamu na wabobezi wa nyanja mbalimbali.

RC Makonda amesema amegundua kuwa wapo mabinti wengi waliofaulu vizuri masomo yao lakini kutokana na wazazi wao kutokuwa na uwezo wa kuwaendeleza kielimu wameishia kupoteza ndoto zao hivyo ameona ni vyema akawaendeleza.

Aidha RC Makonda ameeleza kuwa wasichana hao watagharamiwa kila kitu kuanzia ada,mabegi,vitabu na sare za shule ili wabaki na kazi moja pekee ya kusoma na kufaulu.

Hayo yote yamejiri leo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika ukumbi wa Mlimani City na kuhudhuriwa na Maelfu ya wanawake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...