Jeshi la Polisi
Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu ishirini na moja [21] kwa tuhuma mbalimbali
ikiwa ni pamoja na kufanya shughuli za uganga bila kibali.
KUPATIKANA NA MALI IDHANIWAYO YA WIZI.
Mnamo tarehe 23.03.2019 saa 14:39 mchana huko eneo na Kata ya Ilomba, Tarafa ya Iyunga,
Jiji na Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi walimkamata JOSEPH MGAYA [27] Mkazi wa Ilomba akiwa na Pikipiki MC 395 BYN aina ya Kinglion ambayo mtuhumiwa
amekiri kuiiba Pikipiki hiyo huko Kijiji cha Lupatingatinga Wilaya ya Chunya.
Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika mtuhumiwa
atafikishwa Mahakamani.
KUFANYA
SHUGHULI ZA UGANGA BILA KIBALI.
Mnamo tarehe
25.03.2019 saa 00:10 usiku huko katika Kitongoji cha Mapinduzi 'B' kilichopo katika Kijiji cha Idunda, Kata ya Itewe, Tarafa ya
Tembela, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi walimkamata PASCHAL PATRICE [30] Mkazi wa Kijiji cha Idunda na wenzake 19 wakifanya shughuli ya uganga bila kibali.
Watuhumiwa wote wakiwemo wanawake 03 walikutwa wakiwa kwenye nyumba ya
mtu aliyefahamika kwa jina moja la MWARABU
mkazi wa Dar es salaam. Pia katika nyumba hiyo wamekutwa watu watatu wote
wanaume waliokuwa wamekwenda kutibiwa hapo.
Upekuzi umefanywa ndani ya nyumba
hiyo na kufanikiwa kupata begi ambalo ndani yake likiwa na kibuyu kimoja, chupa
mbili za plastiki zenye unga unaodhaniwa kuwa ni dawa za kienyeji, kikopo cha
plastiki cha njano chenye unga unaodhaniwa kuwa dawa za kienyeji zinazotumiwa
na waganga kutolea tiba pamoja na ngoma moja. Upelelezi unaendelea.
KUSAFIRISHA
BIDHAA NJE YA NCHI BILA KIBALI.
Mnamo
tarehe 24.03.2019 saa 12:15 mchana huko Kitongoji cha Mwambuluko, Kijiji cha Isaki, Kata ya
Katumbasongwe, Tarafa ya Unyakyusa, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa mbeya. Askari
Polisi walikamata gari moja lenye namba T.
268 BNH aina ya Mitsubishi Fuso truck likiwa limebeba magunia yenye nafaka
mahindi makavu yapatao magunia 88 mali
ya mtu mmoja aitwaye DORIN KAONGA [35]
Mmalawi, Mfanyabiashara na Mkazi wa Kalonga - Malawi na GLORY KAFWILA [32] Mmalawi, Mfanyabiashara na Mkazi wa Kalonga - Malawi.
Dereva wa gari hilo alikimbia kusikojulikana na
msako mkali wa kumtafuta unaendelea. Gari hilo lilikua likielekea kivuko haramu
cha Nyasa katika mto Songwe mpakani mwa nchi ya Tanzania na Malawi kwa ajili ya
kuyavusha magunia hayo ya mahindi kwa mitumbwi kuelekea nchi hiyo jirani ya
Malawi.
Gari hilo lililotumika kubeba magunia hayo ya
mahindi ni mali ya mtu mmoja aitwaye SHABAN
ADIL KAJUNI wa huko Wilaya ya
Rungwe. Vielelezo gari hilo na magunia hayo ya mahindi vimekabidhiwa mamlaka ya
mapato idara ya forodha Kasumulu na hatua zaidi za kisheria. Upelelezi
unaendelea.
Imetolewa na:
[ULRICH O. MATEI –
SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
Kivuko haramu kinacjotumiwa na wafanyabiashara wasiokuwa waaminifu kupitisha bidhaa kwenda nje ya nchi.
Magunia ya Mahindi yaliyokamatwa yakisafirishwa kwenda nchi jirani ya Malawi bila kufuata utaratibu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...