Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Chama cha wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu (THTU) kimesema katika kupunguza vifo vya Watoto chini ya miaka mitano nchini, lazima jitihada za kimkakati zichukuliwe katika kupunguza ongezeko la kuzaliwa Kwa watoto wenye ugonjwa wa kichwa kikubwa na mgongo wazi.

Akizungumza na wazazi wa Watoto wenye kichwa kikubwa na mgongo wazi waliopo katika kituo cha Uzima Mission Mwenyekiti wa Kamati ya Wanawake THTU Taifa Salma Fundi amesema katika kusherekea siku ya wanawake wameona kuna umuhimu wa kujua hali ya Watoto wenye matatizo ya kichwa kikubwa na mgongo wazi na kueleza jamii juu ya tatizo hilo na kutaka wadau kuongeza nguvu katika utaoaji wa elimu kwa wanawake pindi wanawake wanapokuwa wajawazito lakini pia utoaji huduma Kwa watoto wenye hali hiyo kwani wanamahitaji mengi. 

Fundi amesema kuwa matatizo ya ugonjwa huu kwa Watoto wakati mwingine hutokana na kukosa elimu juu ya matumizi ya vidonge vya Folic acid, hivyo kama elimu ikitolewa kwa msisitizo tatizo hili linaweza kupungua kuliko ilivyosasa.

Taasisi mbalimbali na Jamii kwa ujumla, lazima tubadilike na kuweka mkakati juu ya Watoto wenye kichwa kikubwa na mgongo wazi ili kufikia malengo yakupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano, kupunguza gharama za matibabu kwa serikali pamoja na umaskini kwani mama mwenye mtoto wa ugonjwa huo huwa hawezi kuzalisha na kubaki tegemezi kipindi chote cha kuuguza.

Katika kuadhimisha siku hiyoTHTU kwa kushirikiana na wadau wengine ( NMB Bank Tawi la Morogoro Road na kampuni ya HQ wamepeleka msaada wa kadi za bima ya Afya kwa Watoto 12, vipima Joto kumi na katoni Moja ya pampers ikiwa ni kuchangia huduma za Afya kwa watoto hao. 

Nae Mratibu wa Chama cha Wazazi wenye Kichwa kikubwa na Mgongo Wazi Hidaya Alawi amesema chama kinawatoto zaidi 1200 ambao hao wamefikishwa katika sehemu za huduma za Afya. Alawi anasema japo kundi kubwa la watoto wenye tatizo hili bado hawajafikishwa kwenye huduma.

Nae Mkurugenzi wa Youth With A Mission Tanzania Jeremiah Kiwinda amesema kuwa baada ya kuona wazazi wanaotoka mikoani na kuja Hospitali ya Muhimbili kwa watoto wenye kichwa kikubwa na mgongo wakaona kuna umuhimu wa kuwapatia malazi na chakula ili kuwaokolea gharama kwa huduma hizo katika Kituo cha Uzima Mission ni Bure.

Amesema kuwa wakiwa katika kituo hicho wanapatiwa mazoezi kwani bila kufanya hivyo kutokana na gharama mbalimbali akiruhusiwa wazazi wengi ni vigumu kurudi.
 Kaimu Katibu wa Kamati ya Wanawake THTU  Roselyne Massam akimkabidhi bima ya afya mmoja ya wazazi wenye watoto wenye Kichwa na Mgongo Wazi katika kituo cha Uzima Mission wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Wanawake THTU Taifa Salma Fundi akipeana na Mkona na mmoja wazazi wenye kichwa kikubwa na Mgongo Wazi ikiwa shukrani ya msaada katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.
 Picha ya pamoja ya wadau waliojitokeza kutoa msaada wakiwa na viongozi wa Kituo cha Uzima Mission na wazazi wenye watoto wenye kichwa kikubwa na mgongo wazi waliokaa chini katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

 Mratibu wa Chama cha wazazi wa watoto wenye kichwa kikubwa na mgongo wazi Hidaya Alawi akizungumza kuhusiana na malezi ya watoto hao na mahitaji wanayotakiwa katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani
Wazazi wenye watoto wa kichwa kikubwa na mgongo wa wazi wakipokea msaada wa pampers  ikiwa ni maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...