Na: Moshy Kiyungi,Dar es Salaam.

Ni hulka ya sisi wanaadamu kusahau mambo mema yaliyofanywa na mazurikumbushana kwa yale mazuri yaliyojiri katika sakafu hii ya Ulimwengu.

Yawezakana kuna baadhi ya watu wameyasahau majina ya Shenazi Salum, aliyekuwa muigizaji na mchezaji wa muziki wa kujitegemea.

Alikuwa kungwi anayefundisha akina mama jinsi ya kuishi na mume hususan kwenye sherehe za kumuaga bi harusi mtarajiwa ‘Kitchen Paty’.
Wasifu wa mwanamama huyo unaeleza kuwa alizaliwa mwaka 1972 jijini Dar es Salaam.

Shenazi alijulikana mno na baadhi ya watu kufuatia 'vimbwanga' vyake alivyokuwa akiviporomosha katika shughuli zake hizo.Alikuwa akiingia ukumbini, watu walikuwa wakizizima kwa nderemo na vifijo, wakimshangilia yeye akipita akijimwayamwaya huku maungo yake yaliyokuwa yamejengeka vyema, yakipishana.

Lakini kwa mapenzi yake mungu, Shenazi alifariki dunia Septemba 08, 2007 katika ajali ya basi iliyotokea kijiji cha Majenje, Mbarali, mkoani Mbeya wakati huo.Alikuwa kwenye basi la SABCO aina ya Scania, T443 APF ambalo liligongana na lori pamoja na magari mawili yanayomilikiwa na Halmashauri ya Mbarali.

Ilielezwa kuwa baadhi ya abiria walikuwa wakimshinikiza dereva wa basi hilo kuongeza kasi ya mwendo, ili wawahi ufunguzi wa Uwanja mpya wa Taifa, ambako kulikuwa na pambano kati ya Taifa Stars na Msumbiji.

Kwa mujibu wa mdogo wa mwanamuziki huyo aitwaye Hanifa Salum, Shenazi alifariki, muda mfupi baada ya kutokea ajali hiyo, iliyohusisha magari matatu na kuua abiria wengine 27.

Aliseme kuwa dada yake Shenazi, alikuwa akirejea nyumbani kwake Dar es Salaam, akitokea katika mji wa Tunduma, alikokuwa akifanya shughuli zake za muziki.“Alituaga kwamba anakwenda Mbeya kufanya ‘shoo’, hatukujua kama ndiyo kifo kilikuwa kinamwita, lakini ndiyo hivyo Mungu kamchukua…”…. alisema Hanifa huku akitokwa na machozi.

Shenazi kwa mara ya mwisho alishiriki katika filamu ya "Kitchen Party", akiwa kama kungwi pamoja na rafiki yake wa karibu aiitwaye Mwajuma Thabiti maarufu kama "Rose Jimama".

Filamu hiyo inaonyesha namna ya kuishi vizuri na mume na mambo mengine mengi tu yenye faida kwa walengwa hususani akina mama.Shenazi alikuwa Malkia wa kunengua miondoko ya Taarab na Mduara nchini, Shenazi

Alikuwa kila aingiapo kwenye ukumbi wowote, hakuwa na soni kujimwagamwaga huku akitikisa maungo yake yaliliyokuwa yamejengeka kike.Rafiki wa Shenazi ambaye naye ni mnenguaji maarufu, Mwajuma Thabit ‘Rose Jimama’, alisema kuwa marehemu alikwenda Mbeya na mwanamke aliyemtaja kwa jina moja la Tuki.

“Nilipata taarifa kama Shenazi amepata ajali, nikapiga simu yake, ikapokelewa na polisi mmoja huko Mbeya. Nikamuomba kuongea na Shenazi, akanijibu, unataka kuongea na maiti? Nilichanganyikiwa, yule polisi aliniambia rafiki yangu Shenazi amekufa, Tuki hali yake ni mbaya, nilidhani utani, lakini yote ni mipango ya Mungu…” alisema Rose kwa uchungu mkubwa.

Habari zaidi zilisema kuwa rafiki huyo wa Shenazi, Tuki, alivunjika miguu yote na alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Misheni ya Chimala, Mbarali.

Mbali na kunengua, malkia Shenazi atakumbukwa kama kungwi maarufu, aliyekuwa akiwafunda watu kabla ya ndoa pia uigizaji wake.

Mungu aipumzishe roho yake pahala pema peponi, Amina.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...