MKURUGENZI Mtendaji wa Benki ya Azania, Charles Itembe, amekutana na wenye hisa wakubwa wa benki hiyo, ambao ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa PSSSF, Hosea Kashimba na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii NSSF  William Erio.

PSSSF inamiliki asilimia 62 ya Benki ya Azania, wakati NSSF inamiliki asilimia 35, hivyo kwa ujumla wake mashirika hayo yanamiliki benki hiyo kwa asilimia 97, ambao ndio wamiliki wakubwa wa Benki hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari, makao makuu ya benki ya Azania, yaliyopo katika jengo la Mawasiliano, barabara ya Sam Nujoma, Dar es Salaam,  Itembe, alisema wanahisa hao walifanya ziara Azania ili kupata kufahamu mchakato unaoendelea wa kuchukua mali na madeni ya bank M.

Bwana Itembe aliwapatia maelezo kuhusu hatua zilizofanyika na matarajio ya baadae kwa wenye hisa hao kwani wamefanya uwekezaji mkubwa.

Mkurugenzi huyo alisema ni vizuri kwa wenye hisa hao kufahamu namna Benki ya Azania itakavyofanyakazi baada ya kuchukua Bank M.

Ikumbukwe Benki Kuu ya Tanzania (BoT) iliamua kuhamisha kwa mujibu wa sheria mali na madeni ya Benki M kwenda Azania Benki Ltd.

Hivyo, kwa sasa BoT na Azania wanaendelea kuandaa taratibu za kisheria za kuhamisha mali na madeni kwenda Azania.

BoT ilikubali Benki M ichukuliwe na Azania kwa ajili ya kuiendesha, ambapo kwa sasa mchakato huo upo hatua za mwisho ili benki hiyo iwe ya Azania moja kwa moja.
Pichani kati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania, Charles Itembe, akifafanua jambo mara baada ya kukutana na wenye hisa wakubwa wa benki hiyo, ambao ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa PSSSF, Hosea Kashimba (kulia)  na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii NSSF  William Erio (kushoto).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...