Michuzi Media Group imepokea taarifa za mshituko na  masikitiko makuwa asubuhi ya leo, kufuatia kifo cha mtangazaji wa habari  wa Clouds FM,Ndugu Ephrahim Kibonde.

Taarifa zinaeleza kuwa Mkuu wa mkoa wa Mwanza ,Mh. John Mongella amethibitisha kufariki kwa mtangazaji huyo kutokana na kudaiwa kusumbuliwa na presha.

Imeelezwa kuwa Kibonde alianza kusumbuliwa na Presha tangu akiwa Bukoba kwenye msiba wa Marehemu Ruge Mutahaba na baadae akahamishiwa Mwanza kwa uangalizi zaidi.

Aidha Mkuu wa vipindi wa Clouds FM,Sebastian Maganga amethibitisha kufariki Dunia kwa Ephrahim Kibonde leo asubuhi katika hospitali ya Bugando,jijini Mwanza.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI-AMEN.
TUTAENDELEA KUWALETEA TAARIFA ZAIDI ,KADIRI YA ZITAKAVYOKUWA ZINATUJIA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...