Na Ripota wa blogu ya Jamii.
KAIMU Mwenyekiti wa klabu ya Yanga SC Samuel Lukumay na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Hussein Nyika wametangaza rasmi leo kujiuzulu nafasi zao.
Viongozi hao wameamua kuachia ngazi mapema ili kupisha mchakato mzima wa uchaguzi mkuu wa klabu unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.
Nyika pamoja na mwenzake Lukumay wameamua kujiondoa ili kutoa mwanya mzuri kwa mchakato wa uchaguzi kwenda vizuri ili kuja kupata warithi wa nafasi hizo.
Aidha hata hivyo licha ya kujiuzulu, Nyika amewaomba msamaha wale wote aliowakosea pindi akiwa madarakani ndani ya klabu hiyo.
''Ninajiuzulu nafasi zangu zote nikiwa kama Mjumbe wa kamati ya utendaji. "Lakini pia Mwenyekiti wa kamati ya usajili na kamati ya mashindano na niombe msamaha kwa wale niliowakosea katika utekelezaji wangu wa majukumu''. Amesema Nyika
Ikumbukwe hivi karibuni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Yanga, George Mkuchika, alitangaza kuwa watakuwa na mkutano mkuu maalum utakaoenda kuamua kama klabu inahitaji kufanya uchaguzi mkuu ama wa kujaza nafasi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...